Gavana Nyoro ateua mgombea mwenza mwenye tajriba ya matibabu

Gavana Nyoro ateua mgombea mwenza mwenye tajriba ya matibabu

NA SAMMY WAWERU

GAVANA wa Kiambu, James Nyoro amemteua Dkt June Njambi Waweru kuwa mgombea mwenza katika uchaguzi mkuu ujao, Agosti 9, 2022.

Akitoa tangazo hilo, Bw Nyoro amemtaja Dkt June kama kiongozi atakayemsaidia kuleta maendeleo Kiambu endapo ataibuka mshindi.

“Katika mchakato wa maamuzi yangu kusaka naibu gavana, usawa kwenye siasa na tajiriba kitaalamu ni kati ya masuala niliyozingatia.

“Dkt June Waweru ana tajiriba pana katika sekta ya matibabu na amefanya kazi kwa karibu na vijana kuhudumia jamii,” Bw Nyoro akaelezea.

Gavana huyo wa Jubilee vilevile alisema uteuzi huo umeafikia usawa wa maeneo Kiambu, akitaja Kiambu Mashariki na Magharibi yamewakilishwa vyema.

Naibu gavana wa sasa Kiambu ni Dkt Joyce Ngugi.

Agosti 6, Bw Nyoroatamenyana na mbunge wa Gatundu Kusini, Moses Kuria wa Chama Cha Kazi, William Kabogo (Tujibebe Party), Kimani Wamatangi wa UDA na mbunge wa Thika Mjini Bw Patrick Kimani Wainaina maarufu kama Wa Jungle (mgombea wa kujitegemea).

Nyoro alimrithi aliyekuwa gavana wa Kiambu Ferdinand Waititu ambaye alibanduliwa Januari 2020, baada ya kuhusishwa na sakata za ufisadi, ubadhirifu wa mali ya umma na matumizi mabaya ya ofisi.

Aidha, Bw Nyoro alikuwa naibu gavana.

You can share this post!

Nafasi ya Joho Azimio kupepeta siasa Pwani

DCI wahoji Sonko kuhusu ghasia wikendi Mombasa

T L