Gavana Sakaja aahidi kuwaajiri maafisa wa kitengo cha usalama

Gavana Sakaja aahidi kuwaajiri maafisa wa kitengo cha usalama

NA WINNIEA ONYANDO

GAVANA wa Nairobi, Johnson Sakaja, ameahidi kuwaajiri maafisa wa kitengo cha usalama 700 ambao kandarasi zao ziliisha chini ya utawala wa Idara ya Huduma za Jiji la Nairobi (NMS).

Haya yanakuja siku chache baada ya waafisa hao almaarufu ‘kanjos’ kuandamana kutaka gavana huyo kutatua suala lao la ajira.

Maafisa hao walidai kwamba walipoteza kazi baada ya NMS kurejeshwa mamalaka kwa serikali ya Kaunti ya Nairobi.

Gavana huyo alisema kwamba maafisa hao wote wataajiriwa katika serikali ya kaunti.

“Nawataka maafisa hao wa kitengo cha usalama wafike kazini mara moja,” akasema gavana Sakaja.

Kadhalika, Bw Sakaja aliwahakikishia wafanyakazi waliokuwa chini ya NMS kwamba hawatapoteza kazi.

“Gharama ya maisha imepanda na haitakuwa haki maafisa hao kufutwa kazi. Kila mmoja anajaribu kutafuta riziki na hii ndio maana nimeagiza warejeshwe kazini,” akasema Bw Sakaja.

Hata hivyo, aliwahakikishia maafisa hao kwamba ikiwa watatuma maombi ya kazi kwa serikai ya kazi watapewa kipaumbele.

Wiki iliyopita, maafisa hao wa usalama waliandamana wakidai malipo ya miezi mitatu.

  • Tags

You can share this post!

Hali ya Man City si shwari tena

Tetemeko: Phoebe Oketch athibitisha yeye na wenzake 2 wa...

T L