Habari Mseto

Gavana wa Nakuru aonya wakazi kuhusu corona

October 2nd, 2020 1 min read

Na Joseph Openda

Gavana wa Nakuru Lee Kinyanjui ameonya kwamba kuna uwezekano kwa kuongezeka kwa visa vya virusi vya corona kufuatia kulegezwa kwa masharti.

Kaunti ya Nakuru ilirekodi visa 24 Jumatano ikifuatiwa kaunti ya Nairobi ambayo ilikuwa na idadi ya juu zaidi ya virusi vya corona. Kulirekodiwa visa 151 vya virusi vya corona.

Visa vingi ambavyo vilirekodiwa kaunti ya Nakuru vilipatikana Nakuru Mashariki, Naivasha, Nakuru Magharibi na Molo.

Kumi kati ya visa hivyo 57 vilivyoripitiwa ni watu ambao wamelazwa kwenye chumba cha watu mahututi.

Gavana Kinyanjui aliwaonya wakazi wa Nakuru akijutia ni kwa nini Rais aliharakisha kufungua nchi  licha ya uwezekano wa kuongezeka kwa maambukizi.

Tafsiri na Faustine Ngila