Gavana Waiguru, Kibicho wazika uhasama

Gavana Waiguru, Kibicho wazika uhasama

Na George Munene

SHEREHE za kuadhimisha Sikukuu ya Mashujaa mwaka huu, zitakazoandaliwa katika Kaunti ya Kirinyaga, zimefanikiwa kuwaleta pamoja mahasimu wakuu Katibu wa Wizara Karanja Kibicho na Gavana Anne Waiguru, kwa sasa.

Rais Uhuru Kenyatta atasafiri kwa ndege hadi eneo hilo Oktoba 20 kuongoza sherehe hizo za kitaifa, ambazo zitafanyika katika uwanja wa michezo wa Wang’uru, eneobunge la Mwea.

Dkt Kibicho na Bi Waiguru mnamo Jumanne walitangaza kukomesha uhasama wa kisiasa kabla ya ziara hiyo kwa heshima ya rais, ili kuhakikisha sherehe zinafanyika kwa amani.

Walitangaza hayo mjini Kutus katika Kaunti ya Kirinyaga na kuongeza kuwa uamuzi huo ni kielelezo cha uongozi bora.

Mkutano huo ulileta pamoja viongozi wa sasa na zamani ikiwemo Seneta Charles Kibiru, Kinara wa Narc-Kenya Martha Karua, Naibu Gavana Peter Ndambiri, na aliyekuwa mbunge wa Ndia Stephen Ngari.

“Tumeafikiana kudumisha amani kwa ajili ya Sikukuu ya Mashujaa. Kama viongozi wa Kirinyaga tunaenzi ushindani wa kisiasa,” alisema Dkt Kibicho.

Waliohudhulia ni pamoja na wabunge Kabinga Wathayu ( Mwea), George Kariuki ( Ndia), Gichimu Githinji ( Gichugu), Munene Wambugu ( Kirinyaga Central) na Mwakilishi Mwanamke Wangui Ngirici ( Kirinyaga).

Seneta Charles Kibiru, Kiongozi wa Narc Kenya Martha Karua, Naibu Gavana Peter Ndambiri , aliyekuwa mbunge wa Ndia Stephen Ngari na Kiongozi wa Wengi katika Bunge la Kaunti ya Kirinyaga Kamau Murango, pia walikuwepo.

‘Tumekubaliana kudumisha amani wakati wa Sikukuu ya Mashujaa. Kama viongozi wa Kirinyaga, tutakuwa na mashindano bora zaidi kisiasa katika eneo hili,” alisema Dkt Kibicho

You can share this post!

CHARLES WASONGA: Serikali izuie wizi wa vyakula vya misaada...

Maseneta wakemea wanahabari kwa kuchapisha video waliyodai...