Bambika

Gen Z mmenipa matumaini kuhusu taifa letu, asema rapa Khaligraph Jones

Na SINDA MATIKO July 4th, 2024 1 min read

RAPA Khaligraph Jones kadai kwamba, alikuwa amekwisha kata tamaa ya kimaisha ila Gen Z wamempa matumaini makubwa sana.

Maandamano ambayo yamekuwa yakiendeshwa na kusukumwa na vijana Gen Z kupinga uongozi mbaya na kupanda kwa gharama ya maisha, yameishia kuzaa matunda huku serikali ikionekana kuwa makini kubadilisha utendaji wake.

Ni hatua hizi ndizo zimeweza kumrejeshea rapa Jones matumaini ya kubadilika kwa maisha Kenya.

“Maandamano yamekuwepo toka zamani dhidi ya utawala dhalimu na gharama za maisha, ila wamekuja hawa na Gen-Z na kubadilisha mchezo kabisa. Nikiwa mkweli kabisa nilikuwa nimekosa matumaini kabisa ya kuja kuwepo na maisha mazuri Kenya ila hawa madogo walichokianzisha wamenifanya kurejesha matumaini yangu na kuona kuwa inawezekana.”

Rapa huyo kwa sasa anasema yupo nyuma ya vuguvugu hilo na ataliungai kadri ya uwezo wake kwani lengo ni kuja kutengenezea mazingira mazuri ya kimaisha sio tu kwa yeye ila kizazi kijacho cha watoto wake.