Gharama ya maisha kero kuu kwa Wakenya-Ripoti

Gharama ya maisha kero kuu kwa Wakenya-Ripoti

Na WANDERI KAMAU

GHARAMA ya juu ya maisha ni miongoni mwa masuala makuu yanayowasumbua sana Wakenya, imeonyesha ripoti mpya iliyotolewa jana.

Kulingana na ripoti hiyo, iliyotolewa na shirika la Infotrak, asilimia 31 ya Wakenya walitaja gharama ya juu ya maisha kuwa tatizo kuu linalowakumba kwa sasa. Walitaja bei za juu za bidhaa za msingi kama vyakula, mafuta na huduma za usafiri kuwa hali zilizochangia gharama hiyo kupanda.

Ukosefu wa ajira ulitajwa na asilimia 15 ya Wakenya, miundomsingi duni (asilimia 15), tatizo la kupata maji safi, ugumu kupata huduma bora za afya kati ya mengine.Akitoa matokeo hayo, Afisa Mkuu Mtendaji wa shirika hilo, Bi Angela Ambitho, alisema Wakenya wengi wanailaumu serikali kuwa kiini cha matatizo hayo.

“Asilimia 35 ya Wakenya wanailaumu serikali kuchangia kudorora kwa uchumi na kupanda kwa gharama ya maisha. Asilimia 32 wanalaumu kiwango cha juu cha ufisadi huku asilimia 20 wakitaja janga la virusi vya corona kuwa sababu kuu,” akasema Bi Ambitho.

Kijumla, asilimia 55 ya Wakenya wanasema mwelekeo wa nchi si wa kuridhisha huku asilimia 16 pekee wakiridhishwa na mwelekeo huo. Matokeo hayo yanajiri huku Wakenya wengi katika maeneo ya mijini wakieleza ugumu kutembeza familia zao katika maeneo ya mashambani kutokana na hali ngumu ya kiuchumi.

“Sitasafiri popote mwaka huu. Nitasherehekea sikukuu za Krisimasi na Mwaka Mpya hapa mjini kwani mwaka huu umekuwa mgumu kwangu sana kifedha. Kila kitu kimepanda bei. Mapato nayo yamepungua katika nyanja zote licha ya serikali kufungua upya uchumi,” akasema Bw Simon King’ori, ambaye ni mfanyabiashara katika eneo la Zimmerman, jijini Nairobi.

Wazazi pia wamekuwa wakilalamika kuathiriwa kifedha na karo ya shule. Mwaka huu, wazazi wengi wamelipa karo mara nne, baada ya serikali kuharakisha ratiba ya sekta ya elimu baada ya wanafunzi kukaa nyumbani karibu mwaka mzima 2020 kutokana na corona.

Licha ya matatizo hayo, Wakenya wengi wamesifia hali ya amani ambayo imekuwepo nchini baada ya Rais Uhuru Kenyatta na kiongozi wa ODM, Raila Odinga, kuondoa tofauti zao za kisiasa kupitia

You can share this post!

Asike imani tele Tusker itaibwaga Homeboyz

Afrika yajadili haja ya mfumo bora wa afya

T L