Githua: Gaspo tunahitaji taji la ligi kuu msimu huu

Githua: Gaspo tunahitaji taji la ligi kuu msimu huu

Na JOHN KIMWERE

MENEJA wa Gaspo Women, Edward Githua amesema wamepania kujituma kiume angalau wahakikishe wameshinda mechi tano zilizosalia za mkondo wa kwanza, kwenye kampeni za Ligi Kuu ya Wanawake (KWPL) ili kujiweka pazuri kuwania taji hilo.

Meneja huyo anahimiza wachezaji wake kuwa msimu huu wanastahili kubeba taji hilo baada ya kumaliza nafasi ya pili mara tatu mfululizo.Gaspo imeibuka ya kwanza muhula huu kuzoa alama moja mbele ya Vihiga Queens baada ya kutoka sare tasa wiki iliyopita.

”Wachezaji wangu wanahitaji wajifunze jinsi ya kumalizia mechi zetu ili kupata mabao maana kwenye mchezo wetu na Vihiga tulipoteza nafasi kadhaa,” meneja huyo alisema na kuwataka wamakinike zaidi dimbani. ”Binafsi nadhani kiasi tumekaa pazuri lakini lazima tushinde mechi zetu zote kama tunahitaji kutawazwa mabingwa wa taji la muhula huu,” akasema.

Aidha anawaonya wachezaji wake kuwa wasibebwe na ufanisi wao kwenye matokeo ya mechi zilizopita bali wapambane mwanzo mwisho kwenye mbio za kupigania taji la muhula huu. Katika jedwali la kampeni za msimu huu baada ya kushiriki mechi sita Gaspo Women ya kocha, Domitila Wangui imeshikilia nafasi ya pili kwa kuzoa alama 13.

Nayo Vihiga Queens ingali kifua mbele kwa kukusanya alama 16.

You can share this post!

Kendia FC ya Ruiru yapiga hatua

Karua aanza mikutano ya kuvumisha Narc-K tayari kwa...

T L