Michezo

Gor Mahia vs Hull City: Vikosi vyatajwa

May 13th, 2018 1 min read

Na GEOFFREY ANENE

HULL City kutoka Uingereza imetangaza kikosi kitakachoanza mechi ya kirafiki dhidi ya Gor Mahia uwanjani Kasarani ambapo mashambulizi yake yataongozwa na Fraizer Campbell.

David Marshall ataanza michumani. Wachezaji wengine watakaoanza dhidi ya mabingwa mara 16 wa Kenya ni Dan Batty, Stephen Kingsley, Robbie McKenzie, Adam Curry, Kevin Stewart, Evandro, mfungaji bora wa Hull simu 2017-2018 Jarrod Bowen, Will Keane na Jon Toral.

Mashabiki wa Gor walianza kumiminika katikati ya jiji la Nairobi mapema Jumapili wakiimba nyimbo na kucheza densi kabla ya kuelekea Kasarani kwa mchuano huu wa kihistoria. Timu hizi zinakutana kwa mara ya kwanza kabisa katika historia yao.

Hata hivyo, mabeki Harun Shakava na Wesley Onguso na kiungo Humphrey Mieno wanafahamu Hull. Watatu hawa walikuwa katika kikosicha timu ya Kenya (SportPesa All Stars) kilichobwagwa 2-1 na Hull    uwanjani K-COM mnamo Februari 27 mwaka 2017.

Mieno alifungia timu hiyo ya Kenya bao safi kutokana na kombora kali nje ya kisanduku.

Muingereza Dylan Kerr, ambaye ni kocha mkuu wa Gor, ametaja Shakava na Mieno katika kikosi kitakachoanza dhidi ya Hull. Boniface Oluoch ataanza michumani.

Wachezaji wengine waliojumuishwa katika kikosi cha wachezaji 11 wa kwanza ni Philemon Otieno, Mganda Godfrey Walusimbi, Joash Onyango, Ernest Wendo, Francis Kahata, Mrwanda Jacques Tuyisenge, raia wa Ivory Coast Ephrem Guikan na George ‘Blackberry’ Odhiambo. Hull City, ambayo inashiriki Ligi ya Daraja ya Pili nchini Uingereza, inanolewa na Nigel Adkins.