Michezo

Gor Mahia wajinasia huduma za fowadi wa zamani wa Thika United

August 29th, 2020 1 min read

Na CHRIS ADUNGO

MABINGWA mara 19 wa Ligi Kuu ya Kenya (KPL), Gor Mahia, wamemsajili fowadi wa zamani wa Thika United, John Macharia.

Macharia ametia saini mkataba wa miaka miwili ambao kwa sasa utamdumisha kambini mwa K’Ogalo kwa hadi mwishoni mwa 2022.

Mbali na Thika United waliotawazwa mabingwa wa KPL mnamo 2008, Macharia amewahi pia kuvalia jezi za FC Kolkheti na FC Saburto nchini Georgia.

Macharia anakuwa mchezaji wa tatu kusajiliwa na Gor Mahia msimu huu baada ya kiungo mvamizi Tito Okello aliyeagana na Vipers United ya Uganda na kipa Levis Opiyo aliyeagana rasmi na Nairobi City Stars almaarufu ‘Simba wa Nairobi’.

Macharia aliyoyomea Georgia mnamo 2017 ambapo alisajiliwa na FC Kolkheti Poti kutoka FC Talanta. Kolkheti wamewahi pia kujivunia huduma za Wakenya Amos Nondi (kwa sasa Dila Gori) na Eric ‘Marcelo’ Ouma (kwa sasa AIK Fotboll).

Mapema mwaka huu, Macharia alishiriki mazoezi na kikosi cha FC Rustavi kinachonogesha Ligi ya Daraja la Pili nchini Georgia.

Gor Mahia wametikiswa pakubwa muhula huu baada ya kuagana na wanasoka wengi wa haiba kubwa akiwemo beki na naibu nahodha Joash Onyango aliyesajiliwa na miamba wa soka ya Tanzania, Simba SC.

Wanasoka wengine ambao tayari wameagana na Gor Mahia ni kiungo mzawa wa Ghana Jackson Owusu, kipa David Mapigano aliyetua Azam FC, fowadi Dickson Ambundo aliyesajiliwa na Dodoma Jiji, mshambuliaji Bonoface Omondi na kipa Peter Odhiambo walioingia katika sajili rasmi ya Wazito FC.

Wanasoka wengine wanaotazamiwa kubanduka kambini mwa Gor Mahia ni nahodha Kenneth Muguna anayehusishwa na Petro Atletico ya Angola, beki Charles Momanyi ambaye yuko pua na mdomo na kutua KCB

Baada ya kutawazwa mabingwa wa KPL msimu huu wa 2019-20, Gor Mahia watapeperusha bendera ya Kenya kwenye kipute cha Klabu Bingwa barani Afrika (CAF Champions League msimu ujao).