Michezo

Gor Mahia yamteua Oruro kuwa Kaimu Afisa Mkuu Mtendaji

October 1st, 2020 1 min read

Na CHRIS ADUNGO

RAYMOND Oruo ameteuliwa kuwa Kaimu Afisa Mkuu Mtendaji wa Gor Mahia.

Kinara huyo atashikilia pia wadhfa wa Afisa Mkuu wa masuala ya mauzo ya na usimamizi wa soka kambini mwa mabingwa hao mara 19 wa Ligi Kuu ya Kenya.

Oruo ameteuliwa na Gor Mahia kujaza pengo lililoachwa na Lordvick Aduda ambaye alijiuzulu ili awanie urais wa Shirikisho la Soka la Kenya (FKF) katika uchaguzi mkuu ujao wa Oktoba 17, 2020.

Katika wadhifa wake, Oruo ambaye ni Afisa Mkuu Mtendaji wa zamani wa Shirikisho la Raga la Kenya (KRU), atakuwa pia Bodi ya Usimamizi ya Gor Mahia na atakuwa chni ya Katibu Mkuu, Sam Ocholla.

Oruo amewahi pia kuwa meneja wa masuala ya michezo katika Benki ya KCB inayojivunia vikosi maarufu vya raga na soka, voliboli katika ulingo wa michezo ya humu nchini.

Gor Mahia wanalenga kujiendeshea masuala yao kitaaluma zaidi baada ya kupitisha Katiba ya klabu inayosisitiza sana umuhimu wa kuzingatiwa kwa mifumo ya uongozini kikosini. Gor Mahia pia wametangaza nafasi za kazi katika afisi ya fedha, uanahabari na masuala ya usalama.