Grandie mpango mzima analenga kufika levo ya Lupita Nyong’o

Grandie mpango mzima analenga kufika levo ya Lupita Nyong’o

Na JOHN KIMWERE

NI kati ya waigizaji wanaoibukia ambao wamepania kujibiidisha wakipania kutinga upeo wa kimataifa miaka ijayo. Anaamini kwamba ndio anaaza kupiga ngoma lakini ana kipaji katika masuala ya burudani.

Sheila Moraa Mogere maarufu Grandie anasema alivutiwa na uigizaji baada ya kutazama filamu iitwayo Disconnect kazi yake Kate the actress. Ingawa anawazia masuala ya uigizaji anatarajia kujiunga na Chuo Kikuu cha Mount Kenya (MKU) kusomea masuala ya uana habari.

”Hakuna haja kupiga kona huko na kule ukweli wa mambo ni kwamba ninapenda kuigiza ingawa sijaanza kuona matunda yake,” anasema na kuongeza kuwa katika mpango mzima amepania kutinga kiwango cha kimataifa kama mwigizaji Lupita Nyong’o anayeendelea kutesa katika filamu za Hollywood. Anasisitiza kuwa malengo yake katika uigizaji ni kwamba watu wakimtazama wanakumbuka miondoko yake.

Perfect Match

Binti anajivunia kushiriki kipindi cha Perfect Match kiliopepererushwa kupitia Ebru TV. Hata hivyo anasema ndoto yake ni kuhitimu kuwa mtangazaji wa runinga. ”Sijafanikiwa kupata ajira ya uigizaji lakini tunashirikiana na wasanii kadhaa ambapo tunatengeneza filamu fupi na kuzitupia kwenye mtandao wa Youtube,” alinena na kuongeza kuwa wamezamia kazi iitwayo Brave Series.

Anafunga kuwa angependa kuanzisha brandi yake lengo kuu likiwa kuchuna kipato pia kuwajenga waigizaji wanaibukia. Dada huyu aliyezaliwa mwaka 2002 anasema licha ya kwamba amepania makubwa katika tasnia ya maigizo. Anadokeza kuwa ndani ya miaka mitano ijayo angependa kuwa msanii mahiri katika kipindi fulani na ikiwezekana katika nchi ya kigeni. ”Ninasema hayo maana ninahisi nina talanta tosha katika masuala ya maigizo,” akasema.

Sheila Moraa Mogere maarufu Grandie…Picha/JOHN KIMWERE

Mercy Johnson

Kwa waigizaji wa humu nchini anasema angependa sana kufanya kazi nao Kate the actress aliyeshiriki vipindi vya ‘Maempress’ ‘Sue and Jonnie’ kati ya filamu zingine. Pia Jackie Matubia aliyewahi shiriki kipindi cha ‘Tahidi Hig’, na sasa anashiriki ‘Zora’ ambacho hupeperushwa kupitia runinga ya Citizen.

Kimataifa angependa kufanya kazi na waigizaji kama Getrude Mwita wa Tanzania aliyeshiriki filamu ya Huba pia mwigizaji nguli mzawa wa Nigeria Mercy Johnson aliyejizolea sifa tele kupitia filamu ya Ghetto Wife.

Harusi yake

Katika masuala ya mapenzi anashikilia kuwa hakuna jambo limewahi mkuta na kumfanya alie lakini anahisi pengine wakati wa harusi yake ndio atamwaga machozi. Anasema ubunifu ni mtihani mgumu lakini unapozoea huwa mteremko kama kumeza mate.

”Itabidi tuwe wabunifu katika masuala ya maigizo ili kupata mkate wa kila siku kwa kuzingatia hakuna ajira za kuajiriwa. Sina shaka kushauri wasanii wanaokuja kuwa ni muhimu kuheshimiana na kusaidiana panapohitajika badala ya kukemeana.”

Aidha anatoa mwito kwa wenzake wasiwe na pupa ya kupata umaarufu katika tasnia ya maigizo. Anasema itakuwa vyema kwa wanadada kuwakwepa wanaume ambao hupenda kuwashusha hadhi kwa kuwataka kimapenzi ili kuwapa ajira. Pia anawahimiza kuwa nyakati zote wanastahili kujiheshimu na kumweka Mungu mbele kwa chochote wanachofanya.

Sheila Moraa Mogere maarufu Grandie…Picha/JOHN KIMWERE

 

You can share this post!

Madume wa KU wataka kushiriki dimba la Afrika Mashariki...

Rusty Gee atumia mziki kupigana na mihadarati pia ubakaji

T L