Habari Mseto

Greenpeace Africa: Miaka 10 ya kutunza mazingira

November 15th, 2018 1 min read

Na BERNARDINE MUTANU

Shirika la kutetea haki za mazingira Greenpeace Africa linaadhimisha miaka 10 baada ya kuzinduliwa.

“Greenpeace Africa inatumia nafasi hiyo kuweka wazi masuala ya mazingira ambayo ni mengi yanayoathiri Afrika,” alisema Mkurugenzi Mkuu wa Greenpeace Africa Bi Njeri Kabeberi.

Bi Kabeberi alisema kampeni kuhusu mazingira inaweza kufaulu tu kupitia kwa ushirika miongoni mwa washikadau tofauti.

Shirika hilo hulinda mto wa Congo (DRC), uvuvi kwa kiwango cha juu eneo la Magharibi mwa Afrika na kilimo eneo la upembe wa Afrika pamoja na kufanya kampeni dhidi ya kawi inayotokana na mafuta Afrika Kusini kwa lengo la kukabiliana na mabadiliko ya hali ya anga.