Michezo

GUMZO LA SPOTI: Man-United kumsajili Mandzukic ili ajaze pengo la mvamizi Lukaku

August 6th, 2019 1 min read

Na MASHIRIKA

MANCHESTER United wako pua na mdomo kukamilisha usajili wa Mario Mandzukic, 33, kutoka Juventus.

Fowadi huyu mzawa wa Croatia anatazamiwa kutia saini mkataba wa miaka mitatu utakaomshuhudia akitia mfukoni kima cha Sh806 milioni kwa mwaka.

Hii itakuwa nyongeza ya hadi asilimia 35 katika mshahara ambao kwa sasa anapokezwa na Juventus.

Juhudi za kusajiliwa kwa Mandzukic zinachochewa na ulazima wa kocha Ole Gunnar Solskjaer kujaza nafasi itakayoachwa wazi na Romelu Lukaku anayetazamiwa kuingia katika sajili rasmi ya Juventus au Inter Milan kufikia Alhamisi.

Masharti

Awali, Man-United waliweka masharti kwamba Lukaku angejiunga tu na Juventus iwapo kikosi hicho kingewapa mshambuliaji Paulo Dybala.

Juventus wamepania sana kuzinadi huduma za Mandzukic ambaye kwa mujibu wa kocha Maurizio Sarri, hana nafasi kabisa katika kikosi kipya anachokisuka.