GUMZO LA SPOTI: Ole Gunnar alizuia mastaa 5 kuaga klabu

GUMZO LA SPOTI: Ole Gunnar alizuia mastaa 5 kuaga klabu

Na JOHN ASHIHUNDU

MANCHESTER, Uingereza

Kocha Ole Gunnar Solskjaer alifanikiwa kuzuia wachezaji watano kuondoka Old Trafford wakati wa msimu wa uhamisho uliomalizika.

Watano hao walitaka kuondoka baada ya klabu hiyo kutangaza kutangaza ujio wa Jadon Sancho, Raphael Varane na Cristiano Ronaldo kwa jumla ya Sh20.5 bilioni.

Kulingana mshirika wa karibu wa kocha huyo, wachezaji waliozuiliwa kuondoka ni Edinson Cavani na Anthony Martial, waliokuwa na mipango na Barcelona na PSG mtawalia.

Wengine waliotaka kuondoka ni Donny van de Beek aliyetaka kujiunga na Everton, Diogo Dalots aliyetaka kujiunga na Borussia Dortmund na kinda Anthony Elanga.

Lakini waliamua kubakia baada ya kocha huyo kuwahakikishia kwamba wataendelea kuwa kwenye mipango yake ya msimu huu mpya.

You can share this post!

Kiunjuri ashauri Ruto ashirikiane na vyama vingine

UDAKU: Usicheze na Georgina, mapambo yake pekee ni bei ya...