Michezo

GUMZO LA SPOTI: Real hawali hawalali wakimwinda Gnabry

October 7th, 2019 1 min read

Na MWANDISHI WETU

GUMZO limeibuka kuwa mshambuliaji wa Bayern Munich, Serge Gnabry alivutia Real Madrid kwa mchezo wake dhidi ya Tottenham Hotspur na sasa inawazia kutafuta huduma zake.

Mchezaji huyu mwenye umri wa miaka 24 alipachika mabao manne katika ushindi wa Bayern wa magoli 7-2 dhidi ya Spurs jijini London na kufikisha mabao matano na pasi nne zilizozalisha mabao katika mechi nane msimu huu.

Ripoti nchini Uhipania zinasema kuwa mchezo wa Gnabry uwanjani Tottenham Hotspur ulivutia Real kiasi cha kumtia katika orodha ya wachezaji itakaotafuta hivi karibuni.

Gnabry alishindwa kuridhisha Arsenal kabla ya kuelekea Werder Bremen alikoonekana na miamba hao wa Ujerumani na kununuliwa.

Amefungia Ujerumani mabao tisa katika mechi 10 tangu kocha Joachim Loew amuite katika timu ya taifa mwaka 2016.