GUMZO: Pogba kutia wino Juve mwezi Julai

GUMZO: Pogba kutia wino Juve mwezi Julai

IMEKUSANYWA NA CECIL ODONGO

JUVENTUS inatarajia Mfaransa Paul Pogba kutia saini kandarasi nao mwezi Julai baada ya pande zote kuafikiana kwa ‘mdomo’ kuhusu kurejea kwa kiungo huyo wa Manchester United jijini Turin.

Duru zinaarifu kuwa Juventus imekubali kumlipa Sh1 bilioni msimu mzima kabla kuongezwa kwa bonasi ya kushinda mechi. Hata hivyo, mengine yanayohusu makubaliano kati ya kiungo huyo na timu hiyo bado yanaendelea kujadiliwa.

Pogba, 24 alikataa ofa kutoka Manchester City na anarejea Juventus ambayo aliichezea kwa muda wa miaka minne tangu 2012 tena baada ya kuondoka Old Trafford.

Aliporejea Man U mnamo 2016, alinunuliwa kwa Sh13 bilioni japo ameondoka Old Trafford kama mchezaji huru mara hizo mbili.

Pogba alishinda mataji manne ya Serie A akiwa Juventus na atashiriki Uefa msimu ujao kwa kuwa Juventus ilimaliza nafasi ya nne msimu uliopita.

  • Tags

You can share this post!

DOUGLAS MUTUA: Kenya itumie ushawishi wake ipasavyo Afrika...

Wakazi wafurahia kukamilishwa kwa daraja la Makupa

T L