GUMZO: PSG tayari kutoa mabunda ili kumleta Mo’ Salah jijini Paris

GUMZO: PSG tayari kutoa mabunda ili kumleta Mo’ Salah jijini Paris

Na JOHN ASHIHUNDU

KLABU ya Paris Saints-Germain (PSG) inajipanga kumsajili mshambuliaji Mohamed Salah wa Liverpool mwenye umri wa miaka 28, endapo nyota wao tegemeo Kylian Mbappe atakataa kuongeza mkataba wake.

Madai haya yametokea siku chache tu baada ya Mmisiri huyo kufunga bao na kuisaidia Liverpool kuibuka na ushindi wa 4-2 dhidi ya Manchester United.

Ushindi ambao ulikuwa wa kwanza wa vigogo hao kuandikisha ugani Old Trafford tangu Machi, 2014.

Kadhalika matokeo hayo yameimarisha ndoto zao za kumaliza miongoni mwa timu nne katika Ligi Kuu ya Premia (EPL) na kufuzu kwa michuano ya Klabu Bingwa barani Ulaya (UEFA).

Lilikuwa bao la 30 kwa nyota huyo msimu huu, na sasa amebakisha mabao manne tu kuwafikia Steven Gerrard, Robbie Fowler na Michael Owen walioifungia timu hiyo mabao 100 katika mechi za EPL.

You can share this post!

DIMBA: Washasema Waswidi: Huyu Alex Isak ndiye Zlatan mpya

Mjanja wa kudandia BBI