• Nairobi
  • Last Updated June 12th, 2024 4:24 PM
Afisa wa polisi aelekeza mtutu wa bunduki mdomoni na kujipiga risasi tatu

Afisa wa polisi aelekeza mtutu wa bunduki mdomoni na kujipiga risasi tatu

Na MWANGI MUIRURI

Afisa wa kiume wa polisi katika Kaunti ya Murang’a alijilipua risasi tatu mdomoni Jumatatu jioni na kujiua papo hapo.

Kulingana na ripoti iliyoandikishwa katika Kitengo cha Upelelezi wa Jinai (DCI) mjini Murang’a, afisa huyo alikuwa anahudumu katika kituo cha polisi cha Nyakianga.

“Haijatambulika sababu kamili ya afisa huyo kufanya hivyo, lakini alijipiga risasi mara tatu mdomoni na kufariki papo hapo,” ripoti hiyo ilisema.

Ripoti ambayo Taifa Leo iliona inaonyesha kwamba afisa huyo wa polisi alionekana kukabiliwa na shinikizo za kiakili, na hakusikiza wenzake waliojaribu kumzuia kujiangamiza.

Ripoti hiyo inaendelea kusema kwamba maafisa wa upelelezi tayari wameshatembelea eneo la kisa na kubeba idhibati kabla ya kupeleka mwili huo katika hospitali ya Misheni ya Kiriaini kwa upasuaji wa maiti.

Kamanda wa polisi wa Murang’a Bw Mathiu Kainga alisema kisa hicho kinaendelea kuchunguzwa na ripoti mahsusi itatolewa kuhusu kilichojiri.

“Tunaendelea kuwasiliana na familia ya afisa huyo, tunaandikisha ripoti zaidi za mashahidi…kwa sasa tunachukulia kisa hiki kuwa cha kujitoa uhai,” akasema.

  • Tags

You can share this post!

Nilidanganywa na Kenya Kwanza, alia Waititu akipigwa na...

Mpesa ya mwanaharakati wa ushoga Chiloba ilitumika kulipia...

T L