• Nairobi
  • Last Updated February 22nd, 2024 12:05 PM
Ashtakiwa kwa kutumia magari ya watu kuchukua mikopo

Ashtakiwa kwa kutumia magari ya watu kuchukua mikopo

Na RICHARD MUNGUTI

MWANAMKE ameshtakiwa kwa kutumia magari ya watu kuchukua mikopo kutoka kwa mashirika ya fedha.

Emily Wanjiku Kimani alishtakiwa mbele ya hakimu mkuu Francis Kyambia kwa makosa ya kughushi stakabadhi za umiliki wa magari.

Mahakama ilifahamishwa kwamba Wanjiku alikuwa anatumia vitabu vya kumbukumbu (logbook) alivyoghushi vya magari na kusajili kwa jina la mtu mwingine na kuvitumia kupokea mikopo.

Mojapo ya shtaka linalomkabili, ni kughushi hati ya umiliki wa gari nambari ya usajili KDA 005M kuwa halisi iliyotolewa na Mamlaka ya Usafiri na Usalama NTSA.

Alidaiwa akishirikiana na watu wengine alighushi cheti hicho cha gari mnamo Juni 2022.

Wanjiku alikana akitumia hati hiyo alipokea mkopo kutoka kwa shirika moja mjini Ruiru, Kaunti ya Kiambu mnamo Aprili 20, 2023.

Alishtakiwa kupeana cheti hicho kwa kampuni ya Keep Vision and Growth Credit Limited ili kupata mkopo.

Wanjiku vilevile alishtakiwa kwa kuandikisha gari nambari KAD 005M lake Bernard Kaniu Kariuki kwa jina la Ann Njeri Kimangu.

Mshtakiwa alikanusha mashtaka dhidi yake na kuachiliwa na Bw Kyambia kwa dhamana ya Sh200, 000.

Kesi hiyo itasikizwa Septemba 6.

  • Tags

You can share this post!

Maina Njenga ahojiwa na DCI, polisi watawanya wafuasi wake

Ashtakiwa kwa kuua mpenzi wake chuoni    

T L