• Nairobi
  • Last Updated December 8th, 2023 10:25 PM
Bandari na Ingwe kupigania pointi KPL Ijumaa

Bandari na Ingwe kupigania pointi KPL Ijumaa

NA ABDULRAHMAN SHERIFF

MECHI ya Ligi Kuu ya Kenya baina ya Bandari na AFC Leopards inayochezwa kesho Ijumaa katika uwanja wa Mbaraki Sports Club mjini Mombasa itakuwa ya majaribio makubwa ya wakufunzi wawili ambao wamejiunga na timu hizo siku za hivi karibuni.

Makocha hao wawili, Andre Cassa Mbungo aliyesajiliwa na Bandari FC mwezi wa Januari, mwaka huu na Patrick Aussems aliye na wiki mbili pekee na timu ya Leopards, wanatarajia kuonyeshana ubabe kila mmoja akitaka kumuonyesha mwenzake ubora wake.

Mbungo aliyekuwa na Bandari kwa muda wa mwezi mmoja unusu, kipindi ambacho timu yake imeweza kupata ushindi kwenye mechi mbili, nyingine mbili kwenda sare na kushindwa mchezo mmoja na Gor Mahia.

Kocha mpya wa AFC Leopards, Patrick Aussems itakuwa ni mechi yake ya pili kuwa katika kikosi cha timu hiyo kwani katika mchezo wake wa kwanza Jumapili iliyopita, aliweza kuiongoza timu yake mpya kushinda mabao 6-0 dhidi ya Tiki FC ya Taveta katika mchezo wa Betway Cup.

Kwa vyovyote vile, mechi hiyo ambayo inatarajia kuwa ya kuvutia na yenye kila aina ya burudani huku mashabiki wakitarajia kuwa majumbani mwao kuishuhudia kupitia kwa stesheni za televisheni za Stars Times na KTN Burudika.

Aussems amesema ana matumaini yake ya timu kupata ushindi dhidi ya Bandari hivi leo. “Nimeishuhudia timu yangu ikicheza mechi dhidi ya Gor na Tiki na nimeona jinsi nitafanya wakati wa mechi na Bandari,” akasema.

Meneja wa Bandari FC, Albert Ogari amesema kuwa wanajiandaa vya kutosha kuhakikisha wamepata ushindi dhidi ya Leopards. “Hatuna tatizo la majeruhi isipokuwa winga wetu Shaaban Kenga ambaye anaendelea na matibabu ya mkuvunjika kwa mguu.

Mechi hiyo inatarajia kuwa ngumu na matokeo yake yatategemea safu ya ushambulizi itakayokuwa bora. Bandari itawategemea zaidi mastraika William Wadri (Mganda), Yema Mwana (DR Congo), Darius Msagha na Abdalla Hassan aliye kikosi cha timu ya taifa ya Harambee Stars.

Kwa upande wa Leopards nao watamtegemea zaidi mfungaji wao Elvis Rupia aliye mchezaji bora wa mwezi wa Desemba 2020 ambaye anatarajia kushirikiana na wenzake kina Jaffari Owiti, Fabrice Mugheni, Austin Odhiambo na Harrison Mwendwa.

  • Tags

You can share this post!

Kimemia alaani ubomozi wa majengo Ol Kalou

Raila amtetea Ruto