• Nairobi
  • Last Updated February 22nd, 2024 1:05 PM
Beki Jurrien Timber aimarisha safu ya ulinzi kambini mwa Arsenal

Beki Jurrien Timber aimarisha safu ya ulinzi kambini mwa Arsenal

Na MASHIRIKA

ARSENAL waliimarisha safu yao ya ulinzi kwa kujinasia maarifa ya beki Jurrien Timber kutoka Ajax ya Uholanzi kwa Sh6.3 bilioni.

Ada ya kusajiliwa kwa difenda huyo ambaye alitia saini kandarasi ya muda mrefu uwanjani Emirates, huenda ilifikia Sh7 bilioni.

Timber, 22, anatarajiwa kutambisha Arsenal ambao idara yao ya nyuma imepigwa jeki na hatua ya beki mahiri William Saliba kurefusha mkataba wake kwa miaka minne zaidi.

“Ni fahari tele kwamba Jurrien amejiunga nasi. Ni beki chipukizi ambaye ana uwezo wa kuwajibishwa popote katika safu ya ulinzi,” akasema kocha Mikel Arteta.

Timber, aliyekuwa pia akifukuziwa na Bayern na Man-United, amechezea Uholanzi mara 15.

Aliwajibishwa katika mechi nne kwenye fainali za Kombe la Dunia za 2022 zilizoshuhudia Uholanzi ya kocha Louis van Vaal ikitinga robo-fainali nchini Qatar.

Timber anakuwa mchezaji wa tatu kusajiliwa na Arsenal muhula huu baada ya kiungo mvamizi Kai Havertz, 24, kutokea Chelsea kwa Sh11.6 bilioni na Declan Rice kukamilisha uhamisho wake kutoka West Ham United kwa Sh18.9 bilioni. Arsenal pia wamefaulu kurefusha mikataba ya viungo Bukayo Saka, 21, na Reiss Nelson, 23, baada ya Granit Xhaka kuhamia Bayer Leverkusen ya Ujerumani kwa Sh3.9 bilioni.

Timber alichezea Ajax mechi 47 katika mashindano yote msimu uliopita, zikiwemo sita za hatua ya makundi kwenye Klabu Bingwa Ulaya (UEFA). Alisaidia Ajax kunyanyua Ligi Kuu ya Uholanzi (Eredivisie) mnamo 2021 na 2022.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

JURGEN NAMBEKA: Wakuu Mombasa watafute jibu kwa wanaozurura...

Tanzia: Afisa wa serikali ya Kilifi auawa kwa kudungwa kisu...

T L