• Nairobi
  • Last Updated May 24th, 2024 12:59 PM
Dai mganga alishauri washukiwa wafunike Sh700, 000 za wizi chunguni ili ziongezeke

Dai mganga alishauri washukiwa wafunike Sh700, 000 za wizi chunguni ili ziongezeke

NA BRIAN OCHARO

MAAFISA wa polisi wamedai kuwa, washukiwa wawili waliohusishwa na wizi wa Sh700, 000 za mwajiri wao walizipeleka kwa mganga ili ziongezeke.

Kwenye hati zilizowasilishwa katika Mahakama ya Mombasa, polisi wamedai washukiwa Zanjabil Musumba Mbururu na Desmol Dust Wamalwa, waliagizwa na mganga kuziweka kwenye chungu bila kukifungua kwa miezi mitatu ili ziongezeke.

Inadaiwa mganga aliwaonya kama wangekaidi ushauri wake, pesa hizo zingegeuka jivu.

Walikana mashtaka mbele ya Hakimu Mkuu Mkazi David Odhiambo, wakaachiliwa kwa dhamana ya Sh300, 000 pesa taslimu kila mmoja.

Imedaiwa walipanga njama na wenzao kumwibia Bw Kumar Prateshkumar Prassana, mnamo Mei 10 na 13, 2023 mtawalia eneo la Changamwe.

Inasemekana Bw Mbururu ndiye alipewa pesa kuzishikilia lakini akatoweka nazo.

Alikamatwa Mombasa huku Bw Wamalwa akikamatwa Mumias, Kaunti ya Kakamega.

Imedaiwa Bw Wamalwa alipohojiwa, alidai alikuwa amempa mzazi wake pesa hizo.

 

  • Tags

You can share this post!

Gachagua asimulia alivyozuru kanisa Kericho nusu ya waumini...

Mwanamume auawa na umati akidaiwa kuiba mihogo  

T L