• Nairobi
  • Last Updated February 29th, 2024 5:56 PM
Demu wa beste yangu ataka tupige mechi ya kisiri ugenini

Demu wa beste yangu ataka tupige mechi ya kisiri ugenini

Mpenzi wa rafiki yangu amekuwa akinipigia simu na kunitumia jumbe za kimapenzi akiomba tuwe na mpango wa kando. Nafikiria kumwambia rafiki yangu lakini sijui kama ataniamini. Nishauri.

Ni wazi kwamba mpenzi wa rafiki yako si mwaminifu. Kama urafiki wenu ni wa dhati unafaa kumwambia ukweli hata kama hatakuamini. Atakapogundua atajua wewe ni rafiki wa kweli.

Jirani amenipagawisha; sili, silali sababu yake

Ninahangaika moyoni kwa penzi la mwanamke jirani yangu. Ninajua hana mpenzi na nimetumia mbinu zote kumpata lakini amekataa. Nifanyeje?

Mwanamke huyo amekataa ombi lako kwa sababu hakupendi. Acha kupoteza wakati wako bure kwa sababu huwezi kumlazimisha akupende. Wanawake ni wengi, tafuta anayekupenda.

Kichuna niliyepangia kuoa ni kiruka njia

Nimemuacha mpenzi wangu baada ya kugundua kwamba ana mwingine. Alikuwa amekubali kuwa mke wangu kwa hivyo nilimtambulisha kwa jamaa na marafiki. Sijui nitawaambia nini tena. Nishauri.

Ni jambo la kawaida kwa uhusiano wa kimapenzi kuvunjika kutokana na sababu mbalimbali. Bila shaka waliojua kuhusu uhusiano wenu watakuuliza. Usione aibu kuwaambia ukweli, wataelewa.

Sasa mtaani wanaeneza uvumi eti natoka na jirani

Kuna mwanamke jirani yangu mtaani anayetaka tuwe wapenzi. Nimekataa ombi lake kwa sababu ni mke wa mtu. Lakini watu mtaani wanaamini sisi ni wapenzi. Nahofia uvumi huo utamfikia mume wake. Nishauri.

Watu wanaoeneza habari hizo wanaweka maisha yako hatarini. Zikimfikia mumewe anaweza kuchukua hatua ghafla. Ushauri wangu ni kwamba uhame mtaa huo haraka ili kulinda usalama na heshima yako.

-Imeandaliwa na Fatuma Bariki

  • Tags

You can share this post!

Pigo jingine kwa Serikali korti ikizima kesi dhidi ya...

Wito wa kujiamini barani Afrika, kujitafutia suluhu ya...

T L