• Nairobi
  • Last Updated February 22nd, 2024 1:05 PM
DK Kwenye Beat asema hapo kwa wash wash humpati

DK Kwenye Beat asema hapo kwa wash wash humpati

Na SINDA MATIKO

MWANAMUZIKI wa injili DK Kwenye Beat amekanusha madai kuwa maisha ya kifahari anayoishi kwa sasa yanatokana na biashara chafu ya ‘wash wash’.

DK hajakuwa akifanya shoo toka ile skendo ya ngono iliyomkuta 2019. Hata hivyo, maisha yake yameonekana kumnyookea siku za hivi karibuni na kuchochea tetesi kuwa fedha zake zinatokana na biashara chafu ya utapeli wa pesa almaarufu wash wash.

“Si kweli! Lazima watu watakuwa wana maswali mengi maana sijakuwa nikipiga shoo tangu 2019 toka sakata ile iliponikuta. Ila watu hawajui mimi nilikuwa nimejipanga. Kipindi nilikuwa napata fedha za shoo, niliwekeza na sasa wanachoona ni matunda ya uwekezaji huo. Kwa hivyo, hizo tetesi si kweli”.

Kwenye sakata hiyo, DK alidaiwa kubaka mrembo mmoja na kumwambukiza zinaa.

  • Tags

You can share this post!

Renson Ingonga ateuliwa Mkurugenzi mpya wa Mashtaka ya Umma

Ndoa mashakani EACC ikitwaa pesa za mahari

T L