• Nairobi
  • Last Updated April 17th, 2024 7:55 PM
EACC yatakiwa kuchunguza mradi wa barabara

EACC yatakiwa kuchunguza mradi wa barabara

NA FARHIYA HUSSEIN

UJENZI wa barabara inayounganisha Shule ya Msingi ya Lake Kenyatta na Uziwa katika Kaunti ya Lamu uliogharimu Sh19 milioni, umezua maswali.

Seneta wa kaunti hiyo, Bw Joseph Kamau ameitaka Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi (EACC) na Idara ya Uchunguzi wa Jinai (DCI) kuanzisha uchunguzi wa kina kuhusu suala hilo.

Seneka huyo alisema hali duni ya ujenzi wa barabara, licha ya uwekezaji mkubwa inaibua mashaka kuhusu uwezekano wa usimamizi mbaya au matumizi mabaya ya fedha.

“Barabara hiyo hiyo ndiyo inayotumiwa na wanafunzi, wiki ijayo wamepangiwa kufungua shule, wataendaje shule?” alihoji Seneta Kamau.

  • Tags

You can share this post!

Kalonzo Musyoka amesota

Gachagua sasa aanza ‘kujisafisha’ kisiasa 

T L