• Nairobi
  • Last Updated May 21st, 2024 8:55 PM
Hapa vitenge na jezi tu: Sababu za Mkuu wa Utumishi wa Umma kuzima wafanyakazi kuvalia suti

Hapa vitenge na jezi tu: Sababu za Mkuu wa Utumishi wa Umma kuzima wafanyakazi kuvalia suti

Na MARY WANGARI

WATUMISHI wa Umma wanatarajiwa kuvalia mavazi yasiyo rasmi kazini kuanzia Jumatano hadi Sikukuu ya Jamhuri, mnamo Disemba 12, kama sehemu ya kukaribisha Kongamano Kuu la Vijana Barani Afrika.

Mkuu wa Watumishi wa Umma, Felix Koskei, Jumanne Desemba 5, 2023 aliwaagiza maafisa wa umma kuvalia jezi za timu maarufu wanazopendelea nchini au barani Afrika.

Kulingana na Bw Koskei, hatua hiyo inadhamiriwa kukaribisha Kongamano hilo almaarufu kama YouthConnekt, litakaloandaliwa nchini katika Jumba la KICC kuanzia Ijumaa.

“Kuanzia Alhamisi hadi Sikukuu ya Jamhuri, tuvalie mavazi yasiyo rasmi, ya mitindo ya fasheni na maridadi kupigia debe mdahalo wa Kongamano la Afrika YouthConnekt ambalo tutajivunia kuandaa kuanzia Disemba 8-11,” alisema Bw Koskei kupitia taarifa mtandaoni.

“Onyesheni moyo wenu kuvalia jezi za timu mnazopenda za Kenya au Afrika iwe ni mchezo wa riadha, Harambee Stars, Shujaa au Malkia. Tujivunie kujikwatua kwa fulana hizo.”

Kongamano hilo litakaloandaliwa kwa ushirikiano na Kituo cha YouthConnekt Afrika na Shirika la Umoja wa Mataifa kuhusu Mpango wa Maendeleo (UNDP) linalenga kuhakikisha Afrika inapiga hatua kufikia 2030.

  • Tags

You can share this post!

Pasta aliyekwama hotelini aomba asaidiwe na Sh370,000

El Nino: Mbunge alalamikia ubaguzi katika usambazaji wa...

T L