• Nairobi
  • Last Updated April 23rd, 2024 4:25 PM
Idadi ya walioaga dunia Shakahola yagonga 150

Idadi ya walioaga dunia Shakahola yagonga 150

NA ALEX KALAMA 

KATIKA siku ya tatu ya awamu ya pili ya ufukuaji wa makaburi ili kutoa miili ya watu waliozikwa katika hali tatanishi kwenye msitu wa Shakahola Kaunti ya Kilifi, maafisa wamepata miili mitano baada ya kufukua makaburi katika shamba linalodaiwa kuwa la mhubiri tata Paul Mackenzie.

Akihutubia wanahabari mshirikishi wa Pwani Rhoda Onyancha amesema idadi ya walioaga dunia imefika watu 150 huku idadi ya wale waliookolewa wakiwa hai ikifikia 72 ikiwa ni baada ya wanaume wawili kuokolewa Alhamisi.

“Siku ya leo tumepata miili mitano baada ya kufukua makaburi na pia tumeweza kuokoa watu wawili,” amesema Bi Onyancha.

Hata hivyo afisa huyo wa utawala amedokeza kuwa idadi ya familia zinazotafuta jamaa zao waliopotea imeongezeka na kufikia 594 huku idadi ya watu waliokutanishwa na familia zao ikisalia 14.

“Kufikia sasa zile familia zimeweza kuchukuliwa chembechembe za DNA bado ni zile 93 na idadi ya wale ambao walikamatwa pia imesalia pale kwa 25 pekee,” amesema Bi Onyancha.

  • Tags

You can share this post!

DPP aomba aliyetapeli wabunge nusu milioni asalie gerezani

Dhambi za Yesu wa Tongaren kulingana na polisi

T L