• Nairobi
  • Last Updated October 2nd, 2023 8:00 AM
Jenerali Ogolla achapa kibarua cha kwanza katika Sherehe ya Kitaifa tangu aapishwe kuwa CDF

Jenerali Ogolla achapa kibarua cha kwanza katika Sherehe ya Kitaifa tangu aapishwe kuwa CDF

NA CHARLES WASONGA

MKUU wa Majeshi ya Ulinzi ya Kenya (CDF) aliyeteuliwa juzi Francis Ogolla mnamo Alhamisi Juni 1, 2023 alitekeleza wajibu wake wa kwanza wakati wa sherehe ya kitaifa.

Jenerali Ogolla ambaye mnamo Mei 14, 2023 alipandishwa ngazi na kuwa mkuu wa majeshi aliongoza wanajeshi walioandaa gwaride katika uwanja wa michezo wa Moi, mjini Embu wakati wa sherehe za 60 za Madaraka Dei.

Sherehe hizo ziliongozwa na Rais William Ruto ambaye pia ndiye Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi yote nchini.

Jenerali Ogolla alichukua nafasi ya Jenerali Robert Kibochi ambaye alistaafu baada ya kutimu miaka 62.

Kwa mara ya kwanza tangu kuteuliwa kwake, Mkuu huyo wa majeshi alimsindikiza Rais Ruto kukagua gwaride la heshima lililoandaliwa na Majeshi ya Ulinzi ya Kenya (KDF).

  • Tags

You can share this post!

Chuo Kikuu cha Mtandaoni kuzinduliwa rasmi mwezi huu,...

Rais Biden aanguka baada ya kuongoza hafla ya kufuzu kwa...

T L