• Nairobi
  • Last Updated March 28th, 2024 8:27 PM
Kafyu katika eneo pana la Chakama yaongezwa kwa siku 30 zaidi

Kafyu katika eneo pana la Chakama yaongezwa kwa siku 30 zaidi

ALEX KALAMA Na FARHIYA HUSSEIN

WAZIRI wa Usalama wa Ndani Prof Kithure Kindiki amesema baadhi ya wafuasi wa mhubiri tata Paul Mackenzie ambaye bado yuko kizuizini wameonekana wakitorokea mbuga ya Tsavo Mashariki na eneo la Galana Kulalu ili kujificha.

Prof Kindiki ameyasema hayo mnamo Alhamisi aliporejea Shakahola ambapo ametangaza kuwa kafyu iliyowekwa eneo hilo na eneo pana la Chakama lenye ukubwa wa ekari 5,000 imeongezwa kwa siku 30 zaidi.

Masharti mengine katika eneo la uhalifu yanaendelea kutekelezwa.

Hatua hiyo imejiri baada ya makaburi zaidi kutambuliwa ndani ya msitu huo huku pia operesheni ya kuwatafuta manusura waliosalia msituni ikipanuliwa hadi maeneo ya mbuga ya Tsavo Mashariki na sehemu za Galana Kulalu.

“Kuna baadhi ya wafuasi wa Mackenzie ambao wameonekana wakiingia katika mbuga ya wanyamapori ya Tsavo Mashariki na maeneo ya Galana Kulalu. Yale tumeyaona ndiyo yamefanya tufikie uamuzi wa kuongeza kafyu kwa siku 30 zaidi. Hili lingali eneo la matukio ya uhalifu hivyo hakuna mtu anayeruhusiwa kuingia isipokuwa maafisa wanaondeleza operesheni,” amesema waziri Kindiki.

Vilevile waziri huyo ameitaka Mamlaka ya Mawasiliano nchini (CA) ifanye iwezalo kuyaondoa mahubiri potovu yaliyokuwa yakitolewa na mhubiri Mackenzie ambayo bado yanapatikana katika mitandao ya kijamii.

  • Tags

You can share this post!

Kenya Kwanza yarai Azimio kurejelea mazungumzo

Omanyala afanya mazoezi nchini Ufaransa kabla ya Rabat...

T L