• Nairobi
  • Last Updated February 22nd, 2024 2:11 PM
Kampeni: IEBC yapendekeza Ruto na Raila wachunguzwe

Kampeni: IEBC yapendekeza Ruto na Raila wachunguzwe

NA CHARLES WASONGA

HUENDA Naibu Rais William Ruto na kiongozi wa ODM Raila Odinga wakafunguliwa mashtaka kwa kosa la kutumia mali ya umma kuendesha kampeni zao za urais.

Hii ni baada ya Tume Huru ya Uchaguzi na Umma (IEBC) kumwandia Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP) Noordin Haji ikimtaka achunguze madai kuwa wawili hao wanavunja sheria kwa kutumia mali ya umma katika kampeni zao za mapema.

Mwenyekiti wa tume hiyo Wafula Chebukati Jumatano, Machi 23, 2022 amemwandikia Bw Haji barua kuhusu suala hilo kufuatia malalamishi ambayo IEBC ilipokea kutoka kwa kiongozi wa chama cha Thirdway Alliance Ekuru Aukot.

“Chama cha Thirdway Alliance iliandikia tume hii Ijumaa, Machi 11,2022 akielezea jinsi wawaniaji wawili wa urais Naibu Rais Dkt William Ruto na kiongozi wa ODM Raila Odinga wanatumia rasilimali za umma kuendesha kampeni za mapema,” akasema Bw Chebukati.

Katika barua yake kwa IEBC, Bw Aukot ambaye alikuwa mgombeaji wa urais katika uchaguzi mkuu wa 2017, alisema ni kinyume cha sheria kwa wawili hao kutumia mali ya umma kuendelea manufaa yao ya kibinafsi na ya kisiasa.

Bw Aukot alisema kwa kutumia rasilimali za umma Dkt Ruto na Bw Odinga wanafaidi zaidi kuliko wawaniaji wengine, jambo ambalo linakiuka kanuni ya usawa.

Bw Chebukati alisema ni kufuatia malalamishi haya ambapo IEBC imemwandikia Bw Haji ikimtaka kuchunguza suala hilo ili kuthibitisha madai hayo.

“Sehemu ya 14 ya Sheria ya Uchaguzi ya 2016 inaharamisha matumizi ya mali ya umma nyakazi za kampeni za kuelekea uchaguzi.”

“Ni kwa msingi huu ambapo tungepewa kuelekeza malalamishi hayo kwa afisi yako kwa sababu yanahusiana na wajibu wako,” Bw Chebukati akasema katika barua yake kwa DPP, Bw Haji.

Hata hivyo, mwenyekiti huyo wa IEBC hakusema lolote kuhusu madai ya Bw Aukot kwamba Dkt Ruto na Bw Odinga wanavunja kanuni za uchaguzi kwa kufanya kampeni za mapema kabla ya kipindi rasmi cha kufanya hivyo hakijatimu.

Katika barua yake kwa IEBC Bw Aukot ambaye ni mwanasheria alipendekeza kuwa wawili hao wazuiliwe kushiriki uchaguzi mkuu wa Agosti 9.

Kulingana na kanuni za uchaguzi, wanasiasa wanapaswa kuanza kampeni siku 90 kabla ya tarehe ya uchaguzi.

  • Tags

You can share this post!

Jinsi makaa spesheli yanavyosaidia kupunguza gharama ya...

Wakenya waanza kuvuna medali michezo ya walemavu ya Dubai...

T L