• Nairobi
  • Last Updated April 19th, 2024 11:55 AM
Kero ya Ndovu: Wakazi wa Ganze wasumbuka kupata fomu za kujaza walipwe fidia

Kero ya Ndovu: Wakazi wa Ganze wasumbuka kupata fomu za kujaza walipwe fidia

NA MAUREEN ONGALA

MBUNGE wa Ganze Kenneth Kazungu amelitaka Shirika la Huduma kwa Wanyamapori (KWS) kurudisha huduma zake mashinani ili kupunguza mahangaiko ya wananchi ambao makazi yao na mashamba yamevamiwa na ndovu.

Amelalamika imekuwa vigumu kwa waathiriwa wa uvamizi wa wanyamapori kupata fidia kwa sababu ya gharama za kusafiri hadi afisi za KWS mjini Malindi.

Chifu wa Mrima wa Ndege, Bw Samson Chai, alisema wakulima pia wanalazimika kugharimia usafiri wa afisa wa kilimo kuja kukagua hasara wakati ndovu wanavamia mashamba yao.

Wadi zilizoathirika zaidi ni Bamba, Ganze na Sokoke.

  • Tags

You can share this post!

Omtatah ataka vipengee tata 13 ving’olewe kwenye...

Riadha za Dunia Budapest: Kiptum na Kosgei kuongoza timu ya...

T L