• Nairobi
  • Last Updated March 28th, 2024 12:48 PM
Kibo Africa yazindua pikipiki ya injini ya 160cc

Kibo Africa yazindua pikipiki ya injini ya 160cc

NA LAWRENCE ONGARO

KAMPUNI ya Kibo Africa imezindua pikipiki mpya ya injini ya ufyonzaji mafuta wa 160cc ambayo imesifiwa kwa kusaidia kupunguza hasara ya utumizi wa petroli.

Mkurugenzi wa kampuni hiyo Bw Huib Van de Grijspaarde, alieleza kwamba waendeshaji pikipiki watafurahia aina hii mpya.

“Nina imani ya kwamba pikipiki mpya tuliyozindua ni ya bei nafuu na haina hasara kwa matumizi yake. Ninawarai wanaotamani kuendesha biashara ya usafiri kujitokeza, na kuinunua,” alisema mkurugenzi huyo.

Watengenezaji wa pikipiki kwa kuunganisha vipuri wanasema pikipiki kati ya 25,000 na 35,000 hutengenezwa kila mwezi kutokana na vipuri vipya, ambapo kati ya mwaka wa 2020 na 2021 pikipiki mpya zilizosajiliwa zilipanda kwa asilimia 15.6.

Kwa sasa Kibo hutengeneza pikipiki 10,000 kila mwaka.

Alisema tayari wamenufaisha wateja wengi ambao walinunua pikipiki hizo kutoka kampuni hiyo.

“Bidhaa zetu tunazounda ni za hali ya juu kwa sababu hazifyonzi petroli sana, na vipuri vyake ni vya bei nafuu sokoni,” alieleza mkurugenzi huyo.

Hafla hiyo ilihudhuriwa na naibu mkurugenzi wa idara ya viwanda Bw Gideon Oele na katibu wa Wizara ya Biashara na Viwanda Dkt Juma Mukhwana.

Katibu huyo alisema hatua hiyo ni ya kupongezwa kwa sababu kampuni hiyo itaunda pikipiki kwa wingi na kufanya wateja wazinunue kwa wingi.

“Ninapongeza kampuni hii ya Kibo Africa kwa kufaidi wateja wengi na pia kuunda bidhaa zilizo katika ubora wake,” alisema Dkt Mukhwana.

Kampuni ya Kibo Africa ilijitosa katika biashara mwaka wa 2017 na inalenga kupanuka zaidi ifikapo mwaka wa 2025.

Kulingana na mkurugenzi wa kampuni hiyo Bw Grijspaarde pikipiki hizo zinaweza kubeba mizigo ya kilo 200 wakati mmoja huku ikitumia petroli ya lita 6.8 hadi 10.4 kwa muda mrefu.

  • Tags

You can share this post!

Kioni asisitiza NDC ya Jubilee iliyoitishwa na mrengo wa...

Waziri Owalo ajitokeza kusaidia majagina wa Gor Mahia

T L