• Nairobi
  • Last Updated February 22nd, 2024 2:11 PM
Kitendawili cha kifo cha Jeff Mwathi kuteguliwa kuanzia Agosti 10

Kitendawili cha kifo cha Jeff Mwathi kuteguliwa kuanzia Agosti 10

NA RICHARD MUNGUTI

UCHUNGUZI wa kubaini kilichosababisha kifo cha mwanafunzi Jeff Mwathi aliyekuwa akisomea upambaji katika taasisi ya Nairobi Institute of Business Studies (NIBS) unatarajiwa kuanza Agosti 10, 2023.

Wakili Danstan Omari anayewakilisha familia ya mwanafunzi huyo amesema upande wa Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP) umeorodhesha mashahidi 35 katika juhudi za kubaini aliyetekeleza mauaji hayo ya kinyama.

Mamake kijana huyo, Bi Anne Mwathi akihutubia wanahabari jijini Nairobi leo Alhamisi, amesema anaamini watajua ni nani aliyetekeleza unyama huo na kwamba haki itatendeka.

Iliripotiwa kwamba Mwathi alifariki baada ya kuanguka kutoka kwa nyumba ya ghorofa ya msanii DJ Fatxo jijini Nairobi mnamo Februari 23, 2023.

Alizikwa nyumbani kwao katika Kaunti ya Nakuru.

  • Tags

You can share this post!

Messi ateua kuhamia Amerika kuchezea Inter Miami licha ya...

Gereza la Eldoret lamulikwa kufuatia kifo cha mahabusu...

T L