• Nairobi
  • Last Updated March 28th, 2024 3:25 PM
Kufikia jana Jumatano idadi ya walioangamia Shakahola ilikuwa 145

Kufikia jana Jumatano idadi ya walioangamia Shakahola ilikuwa 145

NA ALEX KALAMA 

KATIKA siku ya pili ya awamu ya pili ya ufukuaji wa makaburi ili kutoa miili ya watu waliozikwa katika hali tatanishi kwenye msitu wa Shakahola kaunti ya Kilifi, maafisa wanaoendeleza shughuli hiyo Jumatano walipata miili 12 ndani ya msitu huo ambapo miili 11 ilitolewa katika makaburi yaliyofukuliwa huku mwili mmoja ukipatikana tu msituni kwenye shamba linalodaiwa kumilikiwa na mhubiri tata Paul Mackenzie.

Akihutubia wanahabari Kamishna wa Pwani Rhoda Onyancha alisema idadi ya watu walioga dunia imefikia 145 huku idadi ya wale waliookolewa wakiwa hai ikifikia 70 baada ya watu wawili kuokolewa Jumatano.

“Siku ya leo tumepata miili 12 ambapo miili 11 tumeipata baada ya kufukua makaburi na mwili mwingine mmoja tumeupata tu kichakani ukiwa bado haujazikwa,” alisema Bi Onyancha jana Jumatano.

Hata hivyo afisa huyo wa utawala alidokeza kuwa idadi ya familia zinazotafuta jamaa zao waliopotea imeongezeka na kufikia 579 huku idadi ya watu  waliokutanishwa na familia zao ikifikia 14.

“Kufikia sasa zile familia zimeweza kuchukuliwa chembechembe za DNA ni 93 na idadi ya wale ambao walikamatwa ni 25 pekee,” alisema Bi Onyancha.

  • Tags

You can share this post!

Pasta na mwanadada watupwa jela kwa kughushi cheti cha ndoa

Shakahola: Wanaotafuta jamaa wasema ngoja ngoja yaumiza

T L