• Nairobi
  • Last Updated April 25th, 2024 3:34 PM
Madaraka Dei: Kamishna wa Trans-Nzoia awaonya watengenezaji pombe haramu

Madaraka Dei: Kamishna wa Trans-Nzoia awaonya watengenezaji pombe haramu

NA OSBORN MANYENGO

KAMISHNA wa Kaunti ya Trans-Nzoia Gideon Oyagi ameonya watengenezaji wa pombe haramu eneo hilo huku akiwataka waachane na biashara hiyo.

Akihutubia wakazi kwenye hafla ya kuadhimisha Madaraka Dei katika uwanja wa shule ya Bikeke iliyoko kaunti ndogo ya Kiminini Bw Oyagi amesema ni lazima pombe haramu imalizwe kila sehemu Trans-Nzoia huku akiwataka machifu na manaibu wao kufanya misako mara kwa mara.

Bw Oyagi aliwataka wale wote wanaofanya biashara hiyo kuacha kwa hiari bila kusubiri maafisa wa usalama kuwafikia.

Ameonya yule atakayepatikana atachukuliwa hatua kali akiwaambia wajitayarishe maana atashirikiana na maafisa wake kufanya msako wa pombe haramu.

“Nawaonya wale wanaofanya biashara ya pombe haramu waache hiyo biashara kabla niwafikie. Nitahakikisha pombe haramu inaisha katika eneo hili,” amesema.

Aidha Kamishna Oyagi amewahimiza viongozi wa kisiasa Kaunti ya Trans-Nzoia kushirikiana na kufanya kazi pamoja ili kuleta maendeleo kwa wananchi. Amesema amani ni muhimu, akieleza kwamba Trans-Nzoia ni nyumbani kwa watu kutoka makabila mbalimbali na wanafaa kuishi kwa upendo.

Hafla hiyo imehudhuriwa na Gavana wa Trans-Nzoia George Natembeya, mbunge wa Kiminini Maurice Kakai Bisau, madiwani 10 wa Kaunti ya Trans-Nzoia na maafisa kadhaa wa serikali ya kaunti.

  • Tags

You can share this post!

FKF yashirikiana na FIFA kukuza soka ya akina dada nchini

Omanyala atutumua misuli akijiandaa kuwakabili wapinzani...

T L