• Nairobi
  • Last Updated March 28th, 2024 4:31 PM
Majambazi kuona cha mtema kuni Nakuru

Majambazi kuona cha mtema kuni Nakuru

NA RICHARD MUNGUTI

HIVI karibuni majambazi na wahalifu hawatakuwa na mahala pa kujificha jijini Nakuru kufuatia kuwekwa kwa kamera zitakazosaidia polisi kuwaandama wanaotekeleza uhalifu.

Kamera hizo zimewekwa katikati mwa jiji hili ambako ni kitovu cha biashara (CBD).

Kulingana wakuu wa jiji hili, hatua hiyo imechukuliwa kuhakikisha biashara zimeendelezwa masaa 24 bila hofu ya kuibiwa.

Meneja wa jiji la Nakuru Bw Gitau Thabanja amedokeza kuwekwa kwa kamera hizi za CCTV zimewatia wezi kiwewe kwa vile wanajua maisha yao yako hatarini sasa.

Kamera hizi zimelipatia jiji la Nakuru sura mpya itakayolilinganisha na miji mingine mikuu nchini.

Barabara ya Kenyatta Avenue imewekwa kamera hizo na upanuzi unaendelea katika maeneo mengine jijini humo.

Hapo awali wezi wamekuwa wakishambulia benki na kutokomea bila kuonekana lakini kamera hizi zitafanya kazi kwa muda wa saa 24.

Gavana wa Nakuru Susan Kihika amesema utawala wake utarejesha umaarufu wa jiji hili kwa kuhakikisha huduma za biashara zinaendelezwa kwa muda wa saa 24.

  • Tags

You can share this post!

WANTO WARUI: Kuna hatari serikali kujiondoa katika ufadhili...

Kahaba asimulia jinsi mteja alivyogeuka jini na kutoweka

T L