• Nairobi
  • Last Updated October 2nd, 2023 5:50 AM
Mhubiri ashtakiwa kwa ulaghai wa shamba la Sh60 milioni

Mhubiri ashtakiwa kwa ulaghai wa shamba la Sh60 milioni

Na RICHARD MUNGUTI

MMISHENARI kutoka Canada ameshtakiwa kwa ulaghai wa shamba la Sh60 milioni.

Sheppard Nelson Jason aliyeshtakiwa mbele ya mahakama ya Milimani alikana mashtaka matano ya kula njama za kumnyang’anya Jeremiah Muuya Sailoji na mkewe Rhodah Anne Baxter shamba la ektari 6.5.

Alikana mashtaka mbele ya hakimu mkuu Lucas Onyina.

Jason aliomba hakimu amwachilie kwa dhamana akisema “amekuwa akiishi hapa nchini kwa zaidi ya miaka10 na hawezi kutoroka.”

Mshtakiwa alieleza mahakama amejenga makao ya watoto na anawasaidia watoto mayatima 85 wanaoishu katika shamba hilo.

Upande wa mashtaka haukupinga mshtakiwa akiachiliwa kwa dhamana.

Hakimu Onyina alimwachilia kwa dhamana ya Sh200, 000.

  • Tags

You can share this post!

Serikali yatwaa Sh102 milioni alizopokea mwanadada kutoka...

Microsoft ADC yashirikiana na YALI kuwahami vijana na ujuzi

T L