• Nairobi
  • Last Updated October 2nd, 2023 7:00 AM
Migogoro ya kisiasa kati ya magavana na manaibu wao yaenea

Migogoro ya kisiasa kati ya magavana na manaibu wao yaenea

NA WAANDISHI WETU

IMEIBUKA kuwa teuzi muhimu na upendeleo wa kiukoo ni miongoni mwa masuala yanayosababisha vuta nikuvute kati ya magavana na manaibu wao.

Tayari mizozo ya kisiasa inazidi kutanda katika kaunti kadhaa huku magavana na manaibu wao wakirushiana cheche za maneno hadharani.

Hali hii ya viongozi – gavana na naibu gavana – kurushiana maneno hadharani bila kujali umma imeshuhudiwa katika kaunti za Siaya na Kericho.

Ripoti za faraghani pia zimefichua kuwa katika kaunti za Meru na Baringo, magavana na manaibu wao wameanza kuzozana.

Mahojiano na baadhi ya manaibu gavana – ambao baadhi yao walikataa kurekodiwa – yalifichua kwamba mzozo wa kisiasa umeenea.

Manaibu gavana wanadai kuwa mzozo huo ni kwa sababu ya kupuuzwa katika uendeshaji wa kaunti.

Sheria, mbali na kuwataja manaibu gavana kuwa ndio wasaidizi wakuu wa wakubwa wao, haifafanui jukumu lao au maamuzi wanayoweza kufanya wakiwa madarakani.

Inadhamiriwa kuwa, kwa sababu hii, magavana wengi wamepata mwanya wa kuwaepuka manaibu wao, ambao wengi wao wanawaona kama washindani badala ya washirika, katika uendeshaji wa masuala ya kaunti.

Majukumu pekee ambayo yamehusishwa na naibu gavana yamebainishwa katika Kifungu cha 179 (3 na 4).

Naibu Gavana wa Machakos Francis Mwangangi aliambia Taifa Jumapili kuwa mazungumzo yao chini ya Jukwaa la Manaibu gavana yalifichua kuwa wengi wa manaibu hao tayari hawana uhusiano mwema na mabosi wao.

  • Tags

You can share this post!

Arsenal wafika mwisho wa lami

Kaunti yatoa ilani kuzika miili

T L