• Nairobi
  • Last Updated February 22nd, 2024 2:11 PM
Mke hula kupita kiasi, nashindwa kumwambia

Mke hula kupita kiasi, nashindwa kumwambia

Nilioa mapema mwaka huu na bado hatujapata mtoto. Nina tatizo kuhusu mke wangu ambaye hana kazi kwa sasa. Anapenda sana kula na hali yake hiyo inaniharibia bajeti. Naona aibu kumwambia. Nifanyeje?

Wajibu wa mume ni kukimu mahitaji yote ya familia yake. Wewe unashindwa kumlisha mke wako. Je, itakuwaje kwa mahitaji mengine hasa mkipata watoto? Kama unashuku uwezo wako, mwambie wazi mke wako muachane mapema.

Nina umri wa miaka 45, nimechelewa kuoa sasa?

Nina umri wa miaka 45 na bado sijaoa. Nimekuwa nikifurahia maisha ya mapenzi yasiyo na masharti ya ndoa na sioni haraka ya kuoa. Je, nimechelewa?

Uamuzi wa kuoa ni suala la mtu binafsi. Mtu anaweza kuoa ama kuolewa akiwa na umri wowote ule bora tu apate mchumba. Ukioa kabla hujatosha maisha unayofurahia hutaweza kutulia katika ndoa.

Aliniacha nilipofutwa, ameanza kunipigia simu baada ya kuajiriwa upya

Mpenzi wangu aliniacha akidai hakuwa na hisia kwangu. Lakini ninaamini aliniacha alipojua nimefutwa kazi. Nimepata kazi nyingine na ameanza kunipigia simu akiomba turudiane. Nifanyeje?

Mapenzi ya dhati hudumu mambo yakiwa mazuri na yakiwa mabaya pia. Huyo anayefurahia mambo yakiwa mazuri tu hana haja na mapenzi bali anataka kukutumia vibaya. Usikubali ombi lake.

Nilimwacha kwa kuwa na wapenzi wengi ila nashindwa kumsahau

Nilikuwa na mpenzi lakini nikamuacha nilipogundua alikuwa na wengine. Natamani kupata mwingine lakini nashindwa kwa sababu nilimpenda sana na bado namfikiria. Nishauri.

Huwezi kumsahau kwa urahisi mtu uliyempa moyo wako. Utahitaji muda zaidi kumtoa katika mawazo yako ndipo uweze kufungua moyo wako kwa mtu mwingine.
u

  • Tags

You can share this post!

Wetang’ula ‘Papa wa Roma’ ndiye kusema...

Kaunti za Pwani zatakiwa kufunza vijana kuthamini wazee...

T L