• Nairobi
  • Last Updated April 23rd, 2024 11:14 AM
Mkurugenzi taabani kwa kulaghai Jimi Wanjigi shamba

Mkurugenzi taabani kwa kulaghai Jimi Wanjigi shamba

Na RICHARD MUNGUTI

MKURUGENZI wa pili wa kampuni inayodai kuwa mmiliki halisi wa shamba la mwaniaji kiti cha urais mwaka 2022 Jimi Wanjigi ameshtakiwa.

Shamba hilo lililoko mtaa wa Westlands Nairobi, lina thamani ya Sh500 milioni.

Henry Njoroge Njenga alishtakiwa mbele ya hakimu mkuu mahakama ya milimani Lucas Onyina.

Alikanusha mashtaka 24 dhidi yake.

Njenga na Samuel Njuguna Chege wa kampuni ya

Horizon Hills Limited (HHL) wameshtakiwa kwa ulaghai wa shamba.

Njenga na Chege mwenye umri wa miaka 53 wamekana kumlaghai Wanjigi na mkewe shamba hilo lililo katika baraba ya General Mathenge Westlands.

Katika shamba hilo, kumejengwa afisi za kampuni ya Kwacha Group of Companies.

Kiongozi wa mashtaka Anderson Gikunda hakupinga mshtakiwa akiachiliwa kwa dhamana

Onyina alimwachilia mshtakiwa kwa dhamana ya Sh2 milioni na mdhamini mmoja.

Bado washtakiwa wengine David Njenga Samson Kuria, Njenga, Antony Masengo Anabaka, Cissy Kalunde Musembi, Valentine Jelimo Kibire, Lawrence Njogu Mungai, Kepha Odhiambo Okongo na Martin Esakina Papa na Cattwright Jacob Owino hawajafikishwa kortini.

Bw Onyina aliamuru polisi wawakamate washtakiwa hawa na kuwafikisha kortini.

  • Tags

You can share this post!

Mauti Shakahola ni unyama uliopangwa – Kindiki

Gavana Waiguru apambana kumiliki nyumba ya Sh200 milioni  

T L