• Nairobi
  • Last Updated February 22nd, 2024 2:11 PM
Mshukiwa wa ulghai alivyotiririkwa na machozi akililia korti imwachilie  

Mshukiwa wa ulghai alivyotiririkwa na machozi akililia korti imwachilie  

NA RICHARD MUNGUTI

WAFANYA biashara wawili wameshtakiwa kwa kumlaghai raia wa Malawi Dola za Amerika ($)445, 000 (sawa na Sh67,640,000 thamani ya Kenya), wakidai wangemsafirishia bidhaa kutoka mjini Belgrade nchini Serbia hadi Blantyre Malawi.

Selestine Muyoka Wanjala na Mourine Oside Mugarizi walishtakiwa mbele ya hakimu mwandamizi Bernard Ochoi.

Walikana kula njama kumlaghai Thomas Burton Coleman kati ya April 2022 na Julai 2022.

Hakimu aliombwa awaachilie washtakiwa kwa dhamana.

Mugarizi alieleza hakimu kwamba ana mtoto mchanga.

“Niliitwa kuandikisha taarifa kwa idara ya uchunguzi wa jinai (DCI) na sikujua nitafikishwa kortini. Niliacha mtoto. Naomba mahakama iniachilie kwa dhamana,” alisema Mugariza.

Alisema polisi walimwachilia kwa dhamana ya Sh20, 000 na akaomba apewe dhamana sawa na hiyo akisema “nataka kurudi Mombasa kuona mtoto.”

Upande wa mashtaka ukiongozwa na James Gachoka haukupinga ombi la dhamana.

Bw Ochoi aliwaachiliwa kwa dhamana ya Sh500, 000 pesa tasilimu.

Kesi itatajwa Desemba 19, 2023 kwa maagizo zaidi.

  • Tags

You can share this post!

Silvanus Osoro alaumu serikali ya Kenyatta kwa masaibu ya...

Mkenya wa miaka 52 ashtakiwa Amerika kwa kupanga kuua bibi...

T L