• Nairobi
  • Last Updated February 25th, 2024 12:33 PM
Mume anaishi mjini na miye huku mashambani, nahofia atanyakuliwa na vicheche

Mume anaishi mjini na miye huku mashambani, nahofia atanyakuliwa na vicheche

Nimeolewa na nimejitolea kudumisha ndoa yangu. Mume wangu anaishi mjini na nahofia anaweza kunyakuliwa kwani siku hizi wanawake wamekuwa wabaya. Nifanye nini?

Ni jambo la kawaida kwa mtu kutatizika mwenzake wa ndoa akiwa mbali. Ni muhimu uwe ukimtembelea mjini mara kwa mara ili kumkinga na watu kama hao.

Hajanipigia simu tangu ahamishiwe kwingine

Mpenzi wangu ni mwalimu wa shule ya upili. Mwezi uliopita alihamishwa hadi shule ya mbali. Tangu aende hajanipigia simu na nimejaribu kumpigia nikagundua amenifungia. Nifanyeje?

Mpenzi wako amekuonyesha wazi kwamba ameamua kuvunja uhusiano wenu. Inawezekana amekuwa akitafuta jinsi ya kukuacha na sasa amepata nafasi hiyo. Kubali uamuzi wake upate kuendelea na maisha yako.

Juzi nimevutiwa mno na mpenzi wa chuoni kuliko wa sasa, ushauri wako?

Kuna mwanamume aliyekuwa mpenzi wangu tukiwa chuo kikuu miaka mitano iliyopita. Juzi tulikutana ghafla mjini akaniambia bado ananipenda. Nishapata mwingine lakini bado nampenda. Nishauri.

Mapenzi ni suala la moyoni. Kama moyo wako unakuelekeza kwa mpenzi wako wa awali, kubali iwe hivyo. Mwelezee uliye naye kwamba umekutana na wako wa zamani na mmeamua kurudiana. Atakubali uamuzi wako.

Amezoea kukaguakagua simu yangu ila hapendi kabisa nikiishika yake!

Nina mpenzi lakini haniamini, anapenda kukagua simu yangu kila mara kujua ninaowasiliana nao. Ajabu ni kuwa haniruhusu nishike yake na nimeanza kumshuku. Nifanyeje?

Hiyo ni tabia ya mpenzi asiye mwaminifu na ndiyo sababu yeye pia hakuamini. Hatakubali ushike simu yake kwa sababu utagundua ana wengine. Fanya juu chini ujue ukweli ili uchukue hatua inayofaa.

-Imeandaliwa na Fatuma Bariki

  • Tags

You can share this post!

Familia yalia mgonjwa wao kuachwa kwenye ambulansi bila...

Muturi ajipata solemba mwaka mmoja baada ya kusaidia Kenya...

T L