• Nairobi
  • Last Updated May 24th, 2024 12:26 PM
Nakhumicha azitaka hospitali zisiwafukuze wagonjwa wanaotegemea NHIF

Nakhumicha azitaka hospitali zisiwafukuze wagonjwa wanaotegemea NHIF

NA DERICK LUVEGA

WAZIRI wa Afya Susan Nakhumicha amesema Bima ya Kitaifa ya Matibabu (NHIF) inafanya kazi baada ya Wizara ya Fedha kutuma fedha kwa mpango huo.

Akizungumza akiwa katika Kaunti ya Vihiga mnamo Jumamosi, waziri Nakhumicha amezitaka hospitali ambazo zimekuwa zikiwafukuza wagonjwa wanaotegemea kadi ya NHIF ziwahudumie NHIF ikianza kushughulikia malipo ambayo hospitali hizo zinaidai.

Alikuwa kwenye hafla ya uzinduzi wa kituo cha mafunzo kuhusu matibabu ya watoto na ugonjwa wa macho kwenye Hospitali ya Macho ya Sabatia katika kaunti hiyo ya Vihiga. Aliandamana na Kinara wa Mawaziri Musalia Mudavadi.

Waziri hajasema ni kiwango gani cha pesa ambazo zimetumwa.

“Nimepigiwa simu kutoka kwa Wizara ya Fedha leo (Jumamosi) asubuhi nikija kwa hafla hii kwamba pesa zimetumwa,” akasema waziri Nakhumicha.

Ameahidi kwamba atatoa kiwango chenyewe akirudi ofisini kuangalia rekodi.

 

  • Tags

You can share this post!

Kilio cha wapangaji walioahidiwa kumiliki nyumba za Buxton...

Dereva Takamoto Katsuta alenga kumakinika kwenye mbio za...

T L