• Nairobi
  • Last Updated May 30th, 2023 2:01 PM
NAPSA Stars wanayochezea Wakenya Calabar na Odhoji yalemewa Ligi Kuu Zambia

NAPSA Stars wanayochezea Wakenya Calabar na Odhoji yalemewa Ligi Kuu Zambia

Na GEOFFREY ANENE

WAKENYA Shaaban Odhoji na David Owino “Calabar” watalazimika kucheza Ligi ya Daraja ya Pili nchini Zambia ama kuhama baada ya klabu yao ya NAPSA Stars kuangukiwa na shoka Jumapili.

Kipa Odhoji na beki Calabar walianza mechi dhidi ya wenyeji Nkwazi ambayo NAPSA imekung’utwa 1-0.NAPSA ilistahili kushinda mechi hiyo pamoja na ile ya kufunga msimu dhidi ya Nkana hapo Juni 27 na kuomba Younge Green Eagles na Indeni kupoteza michuano yao yote ili iponee kutemwa.

Hata hivyo, NAPSA haikuwa na bahati ilipopoteza mechi yake ya saba mfululizo baada ya Steven Mutama kufungia Nkwazi bao la ushindi dakika ya 67.“Matokeo ya leo (Juni 20) yanashuhudia NAPSA Stars ikisukumwa katika ligi ya daraja ya pili baada ya miaka tisa mfululizo kwenye Ligi Kuu,” klabu hiyo ilitangaza.

NAPSA inakamata nafasi ya 16 kwenye ligi hiyo ya klabu 18. Imezoa pointi 36 kutokana na mechi 33. Nkana anayochezea kiungo mshambuliaji Mkenya Duke Abuya ilifufua matumaini ya kuepuka kupoteza nafasi yake kwenye ligi hiyo baada ya kulima Buildcon 2-0 Juni 19.

Inashikilia nafasi ya 15 kwa alama 41, nyuma ya nambari 14 Indeni kwa tofauti ya ubora wa magoli.Ili kuponea kutemwa, Nkana lazima ipige NAPSA ama kutoka nayo sare katika mechi yake ya mwisho na kuomba Indeni ipoteze dhidi ya Kabwe Warriors inayofukuzia tiketi ya Kombe la Mashirikisho la Afrika.

Katika mechi nyingine iliyosakatwa Jumapili, Green Eagles ilifyeka Forest Rangers 3-1, Prison Leopards ikararua Zanaco 2-1 nao mabingwa wapya Zesco United wakabwaga Young Green Eagles 2-1. Red Arrows na Kabwe zilitoka 0-0.

  • Tags

You can share this post!

Wanaraga wa Chipu waingia kambini Brookhouse dimba la...

KQ yaongeza Sh25 milioni kwenye Safari Rally