• Nairobi
  • Last Updated February 25th, 2024 11:30 AM
Nilimnasa akigawa asali akadai simtoshelezi

Nilimnasa akigawa asali akadai simtoshelezi

Juzi nilimfumania mpenzi wangu na mwanamume mwingine. Ninamwamini sana na tukio hilo limeniacha hali mbaya. Alijitetea akisema simtoshelezi. Nifanye nini?

Kitendo na matamshi ya mpenzi wako yameondoa matumaini yoyote ya uhusiano kati yenu. Kama ametafuta mwingine kwa sababu humtoshelezi huna manufaa yoyote kwake. Achana naye.

Mke anatisha kuniacha sababu ya marafiki

Nimeoa na tuna watoto wawili. Mama watoto ameonya niachane na marafiki zangu la sivyo ataniacha. Huwa tunakutana vilabuni na ananiambia wananiharibu. Nifanye nini?

Yamkini mke wako ameona mienendo inayohatarisha ndoa yenu kwa kutangamana na marafiki zako vilabuni. Sasa itabidi uchague kati ya mke wako na marafiki zako.

Kuna kizungumkuti kwa mrembo ninayewinda

Mamangu hajaolewa na mimi ndiye mtoto wake wa pekee. Kuna msichana jirani yetu ameunasa moyo wangu. Lakini nimegundua babake na mama yangu ni wapenzi.

Hapo kuna shida kubwa. Mpenzi wa mama yako ni kama baba yako na binti yake ni kama dada yako. Kwa sababu hiyo, uhusiano wa kimapenzi kati yenu utakuwa mwiko. Itabidi uachane naye.

Demu ametoweka ghafla na mimba yangu

Nimempa mimba mpenzi wangu na niko tayari kumsaidia kulea mtoto huku tukipanga ndoa. Lakini ametoweka ghafla bila sababu na kukatiza mawasiliano. Nifanye nini?

Mpenzi wako ameamua kwamba hataki kuwa mwenzako maishani. Kumbuka kwamba ametoweka baada ya kumhakikishia utagharamia malezi ya mtoto kisha umuoe. Kubali uamuzi wake.

  • Imeandaliwa na Fatuma Bariki
  • Tags

You can share this post!

Tume ya haki yakatazwa kushiriki kesi Shakahola

Jinsi mkimbiaji Kipchoge alivyopokea shahada ya tunuku ya...

T L