• Nairobi
  • Last Updated February 25th, 2024 10:30 AM
Pasta ashauri wanaume kuwa na zaidi ya mke mmoja

Pasta ashauri wanaume kuwa na zaidi ya mke mmoja

NA FRIDAH OKACHI

MCHUNGAJI Elizabeth Mokoro wa Kanisa la Seventh Day Adventist amesema haoni ubaya wowote na ndoa za mitala, hata baada ya wahusika kufanya harusi.

Mitala ni aina ya ndoa ambapo mume au mke anaruhusiwa kuwa na mchumba mwingine.

Mfumo huo, hata hivyo, unatofautiana sana kulingana na tamaduni na muktadha wa kijamii.

Kwa hayo, Pasta Mokoro amewapongeza wanaume wanaovutiwa na hisia za wanawake, akidai wana thamani kuliko wale ambao wanategemea wake zao.

Katika video ya hivi karibuni kupitia Youtube Makala yake ya Get the point na vilevile TikTok, wakati akizungumza kwenye mkutano na wanaume na wanawake, alipinga kanuni za jamii inayoamini kuwa na mke mmoja.

Semi zake zimezua hisia mseto na kushangaza wengi, hasa kwa kupendekeza wanaume waliooa wana uhuru kuwa na wanawake wengine.

“Kuna mwanamke ameketi hapa…Uwepo wa mchepuko, mpenzi, mke mwenza, mpango wa kando, mkamilifu wangu, wa kudumu, chochote unachochagua kumwita, uwepo wao haubatilishi na kubatilisha agano la kiroho – una mke,” alisema.

Mchungaji huyo amewahimiza wanawake wasiache ndoa zao kutokana na ukafiri au ushawishi wa ibilisi, akidai kwamba kuanzishwa kwa mpango wa kando ni mbinu ya mgawanyiko kati ya wanandoa.

Bi Mokoro alisema wanaume huvutiwa na hisia za wanawake, wengine wakiasharia kuwa na thamani tofauti na wanaume ambao hutafutwa na wake zao.

Alisema mwanamume asiye na washindani kimsingi hana maana, akidokeza kwamba ushindani wa mapenzi ya mtu ni uthibitisho wa kutamanika kwa mwanamume huyo.

“Ukiwa na mwanaume ambaye huna mpinzani naye, basi una mwanaume asiyefaa. Kitu kizuri kinapiganiwa. Ukiona wanawake wanampigania, basi jua una mwanaume wa manufaa. Kwa hiyo cheza kama wewe,” alishauri Bi Mokoro.

Mchungaji huyo alisema kuwa na pete ya ndoa si jambo linaloweza kumzuia mwanamke, akisisitiza umuhimu wa wanawake kuheshimu na kutendea wanaume wao mema.

Pasta Mokoro anajulikana kwa mafundisho yake ya ujasiri na yenye uwazi.

 

  • Tags

You can share this post!

Gavana mkaidi atozwa na Seneti faini ya Sh500, 000

Mateso zaidi serikali ikileta ushuru mwingine wa asilimia...

T L