• Nairobi
  • Last Updated March 29th, 2024 4:10 PM
Raha tele Vihiga wakinyanyua ubingwa wa Ligi Kuu

Raha tele Vihiga wakinyanyua ubingwa wa Ligi Kuu

NA TOTO AREGE

Vihiga Queens iliishinda Gaspo Women 2-1 na kutangazwa mabingwa wa Ligi Kuu ya Wanawake ya Kenya (KWPL) msimu wa 2022/23 kwenye mechi ya mwisho ya msimu jana.

Mechi hiyo iliyochezwa katika uwanja mpya wa Police Sacco jijini Nairobi, haikuwa mechi ya lazima kwa Vihiga kushinda  kwa sababu, tayari walikuwa wametangazwa mabingwa baada ya ushindi wao wa 2-1 dhidi ya Nakuru City Queens wikendi iliyopita.

Wenyeji walipata bao la kuongoza dakika ya 20 kupitia kwa Adrian Birungi kwa kichwa kupitia kona iliyochongwa na kiungo Elizabeth Mutukiza.

Vihiga wangeweza kupata bao la kusawazisha dakika ya 34, lakini mpira wa kona uliopigwa na Bertha Omitta haukuzaa matunda baada ya mpira wa kichwa wa Janet Moraa Bundi kugonga mwamba wa goli.

Dakika nne baadae, Bundi alifunga goli dakika ya 38 na lingine dakika 67 na kuwahakikishia timu yake pointi tatu.

Gaspo ilitumia kurasa zao za mitandao ya kijamii Ijumaa kuthibitisha kwamba wataheshimu mechi hiyo baada ya Jumatano wiki hii kutangaza kwamba hawatacheza dhidi ya Vihiga.

 

Kipa wa Gaspo James Ombeng anasema msimu umekuwa na ushindani mkubwa.

 

“Tuliteleza kutwa ubingwa tulipotoka sare mechi mbili mfululizo. Tulijifunza kutokana na makosa yetu na tunahamishia umakini wetu hadi msimu ujao. Tutarejea kwa nguvu zaidi,” alisema Ombeng.

 

Kocha mkuu wa Vihiga Queens Boniface Nyamunyamuh kwamba kila kitu kimetokea kulingana na mipango yao.

 

“Niko pamoja na ushindi na hili tulilokuja. Kushinda ligi haimaanishi kuwa tulikuwa wakamilifu pia tulikuwa na panda na shuka zetu,” aliongeza Nyamunyamuh.

 

Vihiga walimaliza kileleni mwa jedwali wakiwa na alama 55 huku Gaspo wakiwa na alama 49.

 

Rais wa Shirikisho la Soka la Kenya (FKF) Nick Mwendwa alikabidhi Vihiga kombe nae naibu wa rais Doris Petra akawakabidhi hundi ya Sh1 milioni.

 

Katika uwanja huo huo, mabingwa wa zamani Thika Queens waliilaza Zetech Sparks 1-0 na kumaliza msimu kwa kishindo. Bao hilo la pekee lilifungwa na Grace Wekesa.

 

Kisumu All Starlets walilaza Transzoia Falcons 6-0 katika uwanja wa Moi kaunti ya Kisumu.

 

Beth Achieng, Beverline Adika na Faith Ogeda walifunga mabao mawili kila mmoja. Hata baada ya ushindi huo, Kisumu imeshushwa daraja rasmi kutoka kwa ligi pamoja na Kangemi Ladies na Kayole Starlets.

 

Katika mechi nyingine iliyochezwa katika uwanja wa Mumboha kaunti ya Vihiga, penalti ya Airin Madalina dakika ya 54 ilitosha kuwaokoa Bunyore Starlets kutokana na kushuka daraja dhidi ya Nakuru City Queens.

 

Madalina sasa ndiye mfungaji bora wa ligi akiwa na mabao 18 nyuma ya mshambuliaji wa Thika Queens, Wendy Atieno

  • Tags

You can share this post!

Soko la utalii lapigwa jeki kutokana na wawekezaji wa...

Wanawake wavamia nyumba na kunyakua mume wa wenyewe

T L