• Nairobi
  • Last Updated March 5th, 2024 7:55 AM
Rais atoa ahadi ya kuwainua walemavu

Rais atoa ahadi ya kuwainua walemavu

Na PSCU

RAIS Uhuru Kenyatta amekariri kujitolea kwa serikali katika kuboresha maslahi ya walemavu, akisema watasaidiwa kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa taifa.

Rais, ambaye alizungumza Ijumaa KICC ambako aliongoza kuadhimisha siku ya Umoja wa Mataifa kuhusu Walemavu, alisema walemavu wameendelea kuchukua nyadhifa muhimu za uongozi katika nyanja nyingi ikiwemo siasa.

“Hakika, kote katika siasa, vyama vya kisiasa vimefanya juhudi bayana kuteuwa walemavu katika nyadhifa kuu, pamoja na kutoa kipaumbele kuwateuwa katika nyadhifa zanazopigiwa kura,” akasema Rais.

Ili kuhakikisha kwamba haki za kiafya za walemavu zimelindwa katika mpango unaoendelea wa Afya Bora kwa Wote, Rais aliagiza Wizara ya Afya kuhakikisha huduma za matibabu kuwasaidia walemavu kujimudu katika hali waliyo nayo zinatolewa pia.

You can share this post!

Mkenya ashinda Fukuoka Marathon kwa mara ya kwanza tangu...

Cherono aibuka mfalme mpya wa Valencia Marathon

T L