• Nairobi
  • Last Updated April 23rd, 2024 9:40 PM
Rais Ruto azuru Narok kushiriki sherehe kufurahia Waziri Soipan kujiunga na serikali yake

Rais Ruto azuru Narok kushiriki sherehe kufurahia Waziri Soipan kujiunga na serikali yake

NA MERCY KOSKEI

RAIS William Ruto Jumapili, Juni 4, 2023 amehudhuria sherehe za kumkaribisha nyumbani Waziri wa Mazingira Bi Soipan Tuiya.

Hafla hii ambayo imevutia wanakijiji inafanyika katika kijiji cha Leshuta eneo bunge la Narok Magharibi, Kaunti ya Narok.

Rais ameandamana na Naibu wake Bw Rigathi Gachagua, mkewe Rachael Ruto, spika wa bunge Moses Wetangula na baadhi ya magavana, mawaziri, wajumbe na wawakilishi wadi kutoka pembe zote za nchi.

Bi Tuiya anahudumu kama Waziri wa Mazingira na Usafi tangu 2022 baada ya kutwaa nafasi ya Waziri aliyeondoka Bw Keriako Tobiko.

Bi Tuiya ni mwanamke wa kwanza wa Kimasai kuwa katika Baraza la Mawaziri tangu Kenya kupata uhuru.

Pia amehudumu kama Mwakilishi wa Kike wa Kaunti ya Narok kwa mihula miwili, kabla ya kuwania kiti cha ugavana wa Narok.

Bi Tuiya ni mhitimu wa Shahada ya Uzamili ya Sheria (LL.M) kutoka Chuo Kikuu cha Washington, Amerika, na Shahada ya Sheria kutoka Chuo Kikuu cha Nairobi.

Alipochukua usukani, Bi Tuiya alimshukuru Rais kwa kumpa nafasi uhudumu kama waziri kutoka jamii ya Kimaasai.

“Nashukuru  kila mtu hapa leo kwa kusafiri hadi kijijini nilikozaliwa, ninamshukuru Mungu aliyetupa uhai. Yote yamewezekana kwa uwezo wa Mungu. Ni mungu pekee anayeweza kuchukua msichana mdogo kutoka kijijini na kumweka nilipo, hadithi yangu itakuwa chanzo cha msukumo kwa wengine,” alisema.

  • Tags

You can share this post!

Waziri Kindiki aapa Mackenzie ataozea jela

Waziri Kindiki aonya Azimio kuhusu maandamano

T L