• Nairobi
  • Last Updated February 25th, 2024 11:30 AM
Samidoh ampa mfuasi wake tonge la majibu

Samidoh ampa mfuasi wake tonge la majibu

NA MERCY KOSKEI

MWANAMUZIKI tajika wa nyimbo za Mugithi, Samuel Muchoki maarufu kama Samidoh amewaacha mashibiki wake wanaomfuatilia kwenye mitandao ya kijamii kwa mshangao.

Hii ni baada ya Samidoh kujibu shabiki wake aliyedai kuwa amewekwa na Karen Nyamu.

Baba huyo wa watoto watano alishiriki picha iliyoonyesha msururu wa shoo zake ya mwezi mzima wa Disemba kwa mtandao wake wa Facebook Disemba 2, 2023.

Shabiki mmoja alitoa maoni yake kwa ujasiri kuhusu chapisho hilo, akimwambia kuwa kuna tetesi kwamba alikuwa anawekwa na Karen Nyamu.

Alikuwa akimaanisha kwamba Bi Karen, ambaye ni seneta maalum ndiye ‘humlea’.

Wawili hao wamekuwa kwenye mahusiano haramu, yaliyopelekea Samidoh kuzalisha Karen watoto wawili.

Shabiki huyo aliuliza swali hilo akitaka kujua ikiwa ni kweli alikuwa anawekwa na Karen,  jambo ambalo lilionekana kumkasirisha msanii huyo.

“Na wengine hapa tu wanasema umewekwa,” shabiki huyo akataka kujua.

Nyota huyo wa Mugithi alimjibu shabiki huyo kwa ukali akisema ‘hayupo tena na Nyamu’ na kumwambia ‘amchumbie’ pia.

“Nilitoka sasa, endeni muwekwe pia,” aliandika.

Mashabiki walifurika kwenye safu ya maoni na kutoa hisia tofauti.

“Umechoka haraka sana,” Esther Wanjiku aliandika.

“Samidoh bro (ndugu) utarudi tu nyinyi tumewazoea kukosana mkirudiananga hii jaba,” Mark Kinuthia alisema.

“Hapo hakuna comeback (kurejea),” Vincent Macqwiz aliandika.

Wiki iliyopita tetesi ziliibuka kuwa Samidoh na Karen Nyamu waliachana.

Inasemakana Karen aliacha kumfuata mchumba wake kwenye Instagram.

Samidoh alikuwa mume wa Edday Nderitu, japo waliachana kutokana na uhusiano wake haramu na Karen.

 

  • Tags

You can share this post!

Polo na kahaba wakwamiliana lojing’i Othaya

Wanafunzi wa vyuo wanavyomezea mate mijibaba

T L